Sunday, November 22

UFISADI UPO KILA NCHI.....Waziri mashuhuri Kenya Anne Waiguru ajiuzulu........



Waziri mwenye ushawishi mkubwa katika serikali ya Rais Uhuru Kenyatta amejiuzulu wadhifa wake baada ya shinikizo kutolewa ajiuzulu kutokana na tuhuma za ufisadi.
Bi Anne Waiguru, ambaye amekuwa Waziri wa Mipango na Ugatuzi, amewaambia wanahabari Nairobi kwamba ameshauriwa na daktari wake “achukue muda kupumzika”.
Amewaambia wanahabari kwamba amemwandikia Rais Kenyatta akimtaka amuondolee majukumu yake.
Wakenya wapigania waziri kwenye Twitter
Hata hivyo amesisitiza kwamba hana hatia.
“Ninafuata ushauri wa daktari na nimemuomba Rais aniondolee majukumu yangu kama waziri ... na akiona inafaa, anipe majukumu ambayo si mazito,” Bi Waiguru amesema.

No comments: