Michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika Mashariki na kati maarufu kama CECAFA Senior Challenge Cup yameanza leo November 21 mjini Addis Ababa Ethiopia, ikiwa ni michezo miwili ilikuwa inatarajia kuchezwa leo November 21, timu ya Zanzibar Heroes dhidi ya timu ya taifa ya Burundi ndio zilikuwa timu za kwanza kufungua dimba kabla ya wenyeji Ethiopia watakaocheza dhidi ya Rwanda.
Burundi ambao walikuwa na nyota wao kadhaa akiwemo Didier Kavumbagu anayekipiga katika klabu ya Azam FC ya Tanzania walikuwa wakiutawala mchezo kwa wastani kumiliki mpira kwa asilimia 56 katika kipindi cha kwanza wakati Zanzibar walikuwa na asilimia 44 za umiliki wa mpira kwa dakika zote 45 za kwanza.
Mchezo huo ambao Burundi walikuwa wakifika sana langoni kwa Zanzibar Heroes hadi wanaenda mapumziko walikuwa wanaongoza kwa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Didier Kavumbagu dakika ya 38. Licha ya kipindi cha pili Zanzibar kutafuta nafasi ya kusawazisha goli hilo haikuwezekana.
No comments:
Post a Comment