Tuesday, November 24

ZIARA YA HAPA KAZI TU...KATIBU MKUU KIONGOZI OMBENI SEFUE AFANYA ZIARA MUHIMBILI...

SEF1
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akisisitiza jambo katika mkutano na waandishi wa habari ambao umefanyika leo katika ukumbi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kuhusu utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli kwamba wagonjwa hawapaswi kulala chini. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru. Picha zote kwa hisani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
SEF2
Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue akisaini kitabu cha wageni mara baada baada yakwasili hospitalini hapo.
SEF3
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (katikati) akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ambako amefanya ziara kuangalia utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuhusu huduma bora kwa wagonjwa na kutekeleza wagonjwa kutolala chini. Wagonjwa hivi sasa wanalala kwenye vitanda na siyo chini. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi na Jamii, Dk Donan Mmbando na kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa ya Moi, Othuman Wanin Kiloloma.
SEF4
Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue akihoji kutokamilika kwa mashine ya MRI kwa wakati baada ya kutembelea chumba ambako mashine hiyo imehifadhiwa. Ofisa anayesimamia utengenezaji wa mashine hiyo, Monica ameahidi kwamba mashine hiyo itakamilika Alhamisi ijayo.
SEF5
Mmoja wa mafundi wa mshine ya ST-Scan akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue kuhusu utengenezaji wa mashine hizo. Fundi huyo ameahidi kwamba mashine hiyo itakamilika Jumatano.
Picha zote kwa hisani Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue leo amefanya ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na mambo mengine amesema serikali itaendelea kuboresha sekta ya afya nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati.
 
Akizungumza baada ya kutembelea MNH, Balozi Sefue amesema amekagua mashine za MRI na CT-SCAN na kueleza kuwa spea zimeshafika na kazi ya kutengeneza mashine hizo inaendelea. 
 
Pia amesema kwamba Serikali ya Tanzania imesaini mkataba mpya na Serikali ya Uholanzi wa kununua vifaa vipya na Hospitali ya Muhimbili itapata CT-SCAN moja wakati Hospitali ya Bugando itapata mashine moja ya MRI.
 
Pia, amewataka wahudumu wa afya kuwahudumia vizuri wagonjwa wanaotumia Bima ya Afya ili kuongeza mapato katika hospitali za serikali.
Akizungumzia kuhusu kudhibiti wizi wa dawa za serikali, Balozi Sefue amesema ni vema ukaimarishwa mfumo wa MSD kwa kutumia mifumo ya 
 Tehama na kuwa na maduka yao ya ndani.
 
Katika ziara hiyo, Balozi Sefue amepata fursa ya kufanya kikao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk Donan Mmbando na watendaji wa MNH ili kupata sura ya matatizo yote katika hospitali hiyo.

No comments: