Kobe alitangaza Jumapili kwenye tovuti ya Wachezaji ‘kwamba ameamua kustaafu baada ya msimu huu , huku akiandika kwamba ” msimu huu ndio pekee uliobakia kwangu wa kuwapa nilichonacho. ”
Kobe aliandika kwa mtindo wa shairi huku akiliita “Dear Basketball” na ndani yake kukiwa na maneno kadhaa ya kugusa moyo wa kila mpenda michezo.
Mojawapo ni kauli ya “huu ndio mchezo uliompa na kumtizimia ndoto mtoto aliyekuwa na umri wa mika 6 (akimaanisha mtotoyeye) tu ya kuchezea Lakers na nitaupenda kwa hilo siku zote.”
” Lakini siwezi kukupenda kwa dhati ile kwa muda mrefu, ” Bryant aliandika. ” Msimu huu ndicho ambacho mimi nimebakiwa nacho ambacho naweza kutoa. Moyo wangu unaweza kabisa kukabiliana na vurugu .
Mawazo yangu yanaweza vyema kushughulikia misuguano lakini mwili wangu unajua ni wakati wa kusema kwaheri. “Na hiyo ni sawa . Mimi niko tayari ili uondoke uende zako mmpenzi basketball . ”
Kocha wa Lakers Bryon Scott alisisitiza kuwa Kobe Bryant atacheza mchezo wa Jumapili ambayo itakuwa jumatatu alfajiri kwa Afrika Mashariki. Katika taarifa yake Scott alisema ni kweli kuwa Bryant atastaafu lakini sio kwamba hatocheza maana amesema kuwa ni msimu wake wa mwisho na ataucheza kwa nguvu zote ikiwezekana.
“Nadhani yeye bado anaupenda sana mchezo huu ,” Scott aliwaambia waandishi wa habari . “Kiukweli bado ana shauku kubwa kwa ajili yake na kikubwa bado ni kijana mwenye ushindani wa hali a juu.
” Scott alisema alikuwa ” alistushwa ” wakati Bryant anampa taarifa yake Jumamosi usiku kwamba alikuwa anaenda kutangaza kustaafu kwake siku inayofuata.
“Alinistua aliponiletea taarifa hiyo kiasi fulani,” Scott alisema. Pengine nitakuwa mtu ninayesikitika kwa hili kuliko mtu yoyote mwingine au kitu chochote kile. Mtu ambaye nina mapenzi makubwa sana kwake na mtu ambaye nimekuwa nikiheshimu sana uwezo wake.
Siku zote huwa ni vigumu sana mtu wa kariba ya Kobe katika mchezo akiamua kutundika kila kitu” Hata hivyo mara kadhaa Kobe alikuwa akinukuliwa kwa kuelezea kuwa alifikiri huu ungeweza kuwa msimu wake wa mwisho.
Na kwa kuzingatia namna alivyoanza msimu kwa kiwango kibovu sio jambo geni sana lakini kwa rekodi, uwezo na jina alilojijengea katika NBA ni wazi kuwa ni taarifa kubwa sana.
Kobe Bryant ameshinda kila kitu katika NBA. Akicheza kwa miongo miwili yaani miaka 20, ameshinda tuzo ya MVP, kashinda mmedali zadhahabu za Olympic, kashiriki NBA All Star mara 17, ameshinda ubingwa wa NBA mara sita, kashinda tuzo za MVP za All star.
Hakuna alichobakisha au pointi zake 81 alizofunga katika mchezo mmoja. Pia ni mchezaji wa tatu aliyefunga pointi nyingi zaidi katika NBA.
Kamishna wa Ligi kuu ya kikapuMarekani, Adam Silver naye alitoa maoni yake kwa kusema awe anagombea ubingwa wa NBA, au akiwa katika uwanja tupu wa mazoezi akijaribu kurusha mitupo yake, Kobe Bryant anabaki kuwa mchezaji na mtu mwenye Upendo mkubwa kwa mchezo huu.
No comments:
Post a Comment