Tanzania imedhihirisha kuwa ni tajiri mkubwa wa rasilimali ya gesi
asilia baada ya kugundulika kwa gesi nyingine katika bonde la mto Ruvu
yenye ukubwa wa ujazo wa futi trilioni 2.17.
Ugunduzi huo wa gesi
asilia umefanywa na Kampuni ya Dodsal Hydrocarbons and Power Tanzania
Limited ambayo imekuwa inafanya shughuli za utafutaji wa gesi na mafuta
katika Mkoa wa Pwani.Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Pilavullathil
Surendran alisema jana katika mkutano wa wawekezaji wa gesi na mafuta
ulioandaliwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
kuwa, thamani ya gesi iliyoko katika eneo hilo inafikia Dola za Marekani
bilioni sita sawa na Sh trilioni 12.
Ugunduzi huo mpya unafanya hadi sasa Tanzania kuwa na amana ya gesi yenye ukubwa wa futi za ujazo trilioni 57.27.
No comments:
Post a Comment