Thursday, February 25

SOMA HII......TANZANIA na "Cash Budget"......

Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli, imeamua kutumia mfumo wa ‘Cash Budget (kutumia kilichokusanywa), huku baadhi ya wachumi wakisema utaleta nidhamu ya matumizi ya serikali na kubana watumishi ambao walizoea kutumia vibaya fedha za umma kwa kuzipangia matumizi yasiyo na tija.
Wizara ya Fedha na Mipango imeeleza kuwa, mfumo wa kupanga na kutumia kinachokusanywa na Mamlaka ya Mapato (TRA), ndiyo ulioamuliwa kutumiwa na serikali ya awamu ya tano.Itakumbukwa kuwa, tangu Novemba mwaka jana, mapato ya TRA yalipanda kutoka wastani wa Sh. bilioni 800 na Sh. bilioni 900 kwa mwezi mpaka Sh. trilioni 1.3, Desemba, mwaka jana Sh. trilioni 1.4, Januari, mwaka huu Sh. trilioni 1.06 na malengo ya Februari ni kukusanya Sh. 1.03.
Jana Ofisa Habari wa Wizara ya Fedha na Mipango, Ingiaheddi Mduma, alisema utaratibu wa kutumia kilichokusanywa utaendelea kutumika kila mwezi.
Alisema kila makusanyo yatakayopatikana kwa mwezi husika, yatatumika kulingana na mahitaji husika ya mwezi huo.
“ Mahitaji yakiwa mengi katika mwezi husika, basi hata fedha itakayokusanywa kwa mwezi huo itatumika kulingana na mahitaji hayo, tutakuwa tunafanya hivyo kila mwezi,” alisema Mduma.

No comments: