Klabu ya Manchester City usiku wa September 22 ilikaribishwa na klabu ya Sunderland katika uwanja wa Stadium of Light kucheza mchezo wa Kombe la Capital One, mechi imemalizika kwa klabu ya Manchester City kuibuka na ushindi wa goli 4-1.
Manchester City ikiwa ugenini katika uwanja wa Stadium of Light imeibuka na ushindi wa magoli hayo kupitia kwa mchezaji wake wa kimataifa wa Argentina Sergio Aguero baada ya kupiga penati safi dakika ya 9 ya mchezo, goli la pili lilifungwa dakika ya 25 kupitia kwa Kevin De Bruyne baada ya kutumia vizuri pasi aliyoipata kutoka kwa Raheem Sterling.
Goli la tatu Sunderland walijifunga baada ya Raheem Sterling kupiga shuti kali lililogonga mwamba na kurudi na kumgonga golikipa wa Sunderland Vito Mannone na kuingia nyavuni dakika ya 33. Wakiwa bado wanajiuliza nini kilichotokea Raheem Sterling dakika ya 36 akahitimisha idadi ya magoli 4, Sunderland baada ya kuonyesha jitihada ambazo ziliwasaidia kupata goli moja la kufutia machozi kupitia kwa Toivonen dakika ya 83 ya mchezo.
Matokeo ya mechi nyingine za Capital One zilizopigwa September 22
Hii hapa ni video ya Magoli Sunderland Vs Man City
No comments:
Post a Comment