Wednesday, September 23

ALIKIBA AFUNGUKA JUU YA RAIS AJAYE ANAYEMKUBALI, MCHEKI HAPA RAIS WAKE YEYE 2015


Ali K 5 

Wakati tukishuhudia wasanii kama kalla jeremiah, jack line wolper,Roma mkatoliki na wengineo wakiwa na mwelekeo wa kumshabikia mgombea urais kupitia ukawa yaani Edward Lowassa, huku pia JB,Aunty Ezekiel, Ray, Bi mwenda na wengineo nao wakimuunga mkono mgombea urais kupitia CCM John Pombe Magufuli, sasa rasmi msanii Ali Kiba nae amejiunga rasmi na kina Ray kumpa nguvu magufuli.

 
Ni mwezi mmoja umebaki kufikia siku nyingine kubwa kwa Watanzania kupiga kura kumchagua Rais wanaemtaka, Wabunge pamoja na Madiwani kwenye Uchaguzi mkuu utakaofanyika October 25 2015.

Tayari mpaka sasa tumeona Mastaa mbalimbali wa Tanzania ambao hawajaficha hisia zao ni nani wanamkubali zaidi kwenye kumpa uongozi wa nchi na nafasi nyingine zinazogombaniwa.

basi 

Mwimbaji staa wa bongofleva Ali Kiba ameungana na mastaa wengine kama Diamond Platnumz, Wema Sepetu, Steve Nyerere, Aunty Ezekiel, Ray ‘Vicent Kigosi’ na wengine kuiunga mkono CCM na mgombea wake Urais ambaye ni Dr. John Pombe Magufuli.

Pamoja na kwamba Ali Kiba ameonekana kwenye headlines za kampeni za CCM, hakuwahi kuandika au kupost chochote kwenye kurasa zake kuhusu kiongozi gani anaeona ni sahihi kwake ila sasa ndio amefanya maamuzi hayo kwa mara ya kwanza.

Ali Kiba aliandika kwenye page yake ya Instagram >>> ‘Chaguo langu sahihi MAGUFULI #hapakazitu #KingKiba na kisha Kiba baadae akaweka picha nyingine ya Dr. Magufuli na kuandika ‘ MAGUFULI #hapakazitu #KingKiba‘

No comments: