Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

Friday, October 7

CHAMA CHA WANANCHI {CUF} HATARINI KUFUTWA


Mgogoro unaoiandama CUF huenda ukailetea balaa zaidi, baada ya kuwapo kwa taarifa kuwa huenda ikafutwa kama itazidi kukomalia msimamo ilionao wa kutotaka ushauri.

Thursday, March 10

RAIS WA ZANZIBAR NA VIETNAM WAFANYA MAZUNGUMZO DAR


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akisalimiana na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang, jana Ikulu Jijini Dar es Salaam akipofika kwa mazungumzo na ujumbe aliofuatana nao,Picha na Ikulu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Ujumbe wake (kushoto) wakiwa katika mazungumzo na Ujumbe wa Rais wa Vietnam Truong Tan Sang jana Ikulu Jijini Dar es Salaam akiwa nchini kwa ziara ya Kikazi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto)akifuatana na Rais wa Vietnam Truong Tan Sang(katikati) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jana Ikulu Jijini Dar es Salaam(kulia) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Augustin Mahiga.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)akiagana na mgeni wake Rais wa Vietnam Truong Tan Sang(kushoto) baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jana Ikulu Jijini Dar es Salaam(katikati) mawair mbali mbali wa Vietnum walioungana na Rais Truong

KUBENEA AKAMATWA NA JESHI LA POLIS AJUMUISHWA KESI YA UCHAGUZI WA MEYA DAR


MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea amekamatwa na Jeshi la Polisi leo asubuhi wakati akiwa katika Mahakama ya Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.

Kubenea amekamatwa na polisi akituhumiwa kushiriki kumpiga Terresia Mmbando, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Mmbando alikuwa mwenyekiti wa mkutano wa kumchagua Meya wa Jiji la Dar es Salaam uliofanyika wiki mbili zilizopita na baadaye kuahirishwa hatua ambayo iliibua malumbano.

Kubenea  alikwenda leo mahakamani kuendelea na kesi yake inayohusu kumtukana Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Kesi hiyo ilifunguliwa tarehe 15 Desemba mwaka jana baada ya wawili hao kukutana kwenye Kiwanda cha Nguo cha TOOKU kilichopo Ubungo, jijini Dar es Salaam.

Katika tuhuma za kumpiga Mmbando, waliokamatwa katika hatua ya kwanza ni Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Mwita Waitara, Mbunge wa Ukonga na madiwani wawili ambao kwa sasa wapo nje kwa dhamana.

Baada ya kupata dhamana Mdee alisema “Watake wasitake wataachia, hapa ni Ukawa tu. Yote haya yana mwisho lakini wajue kuwa namba ‘zinatufeva’ na si vinginevyo.”

Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar s Salaam ndio chanzo cha kukamatwa kwa Kubenea na wengine waliotangulia ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimekuwa vikisigana.

Ukawa wanalalamika kuminywa na Halmashauri ya Jiji kwa madai ya kushirikiana na CCM. Ukawa wameeleza kuwa zinafanyika hujuma ili CCM ishinde Umeya wa Jiji.

Jumla ya wajumbe wa mkutano wa kumchagua Meya wa Jiji ni 161. Kwa upande wa Kinondoni kuna wajumbe 58 ambapo CCM wapo 20 na ukawa 38.

Temeke jumla ya wajumbe 49, CCM wapo 31 na ukawa 18 na Ilala jumla ya wajumbe 54 huku CCM wakiwa 23 ukawa 31.

Thursday, November 19

HUYU HAPA NDIYO WAZIRI MKUU WA TANZANIA KUTOKA BUNGENI..2015....

BREAKING NEWS: Mh. Kassim Majaliwa Mbunge wa Ruangwa amependekezwa na Rais John Magufuli kuwa Waziri Mkuu mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Waziri Mkuu aliyependekezwa Mh. Kassim Majaliwa ni mbunge kupitia jimbo la Ruangwa na ana umri wa miaka 54.

Thursday, September 24

WAISLAMU WA MOROGORO WAICHARUKIA SIASA WASEMA MISIKITI SIYO SEHEMU YA KAMPENI




Katika kuadhimisha sikukuu ya Iddi el haji mkoa wa Morogoro viongozi wa dini ya kislamu wamesema misikiti sio mahala pa kampeni za kisiasa na hawapo tayari kuona nyumba za ibada zinatumika kama madaraja ya kuwavusha wanasiasa. 

Wednesday, September 23

ALIKIBA AFUNGUKA JUU YA RAIS AJAYE ANAYEMKUBALI, MCHEKI HAPA RAIS WAKE YEYE 2015


Ali K 5 

Wakati tukishuhudia wasanii kama kalla jeremiah, jack line wolper,Roma mkatoliki na wengineo wakiwa na mwelekeo wa kumshabikia mgombea urais kupitia ukawa yaani Edward Lowassa, huku pia JB,Aunty Ezekiel, Ray, Bi mwenda na wengineo nao wakimuunga mkono mgombea urais kupitia CCM John Pombe Magufuli, sasa rasmi msanii Ali Kiba nae amejiunga rasmi na kina Ray kumpa nguvu magufuli.

Monday, July 13

Afisa usafirishaji ajitosa kuwani Udiwani kata ya Luhota jimbo la Kalenga

KATIBU wa uchumi na fedha wa chama cha usafirishaji Mkoani Iringa, Obedi Luhwago ameamua kujitisa kuwania udiwani katika kata ya Luhota, jimbo la Kalenga wilayani Iringa kwa tiketi ya Chama Cha Mapnduzi (CCM).

Sunday, July 12

SOMA HII ITAKUSAIDIA KUEPUKANA NA UPOTOSHWAJI WA WANASIASA UCHWARA

MUHTASARI WA TAARIFA YA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KUHUSU UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM YA MWAKA 2010 HADI  2015  KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO (OKTOBA 2010 HADI JULAI 2015)



-----------------------------------



DKT. JOHN POMBE MAGUFULI

1
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Dkt. John Pombe Magufuli, mara baada ya kutangazwa kuwa ndiye Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Dodoma Convition Centre, Mjini Dodoma. Dkt. Magufuli ameibuka kidedea kwa jumla ya kura 2104, wakati wapinzani wake Amina Salum Ally, akiibuka na kura 253 na Dkt. Asha-Rose Migiro, akipata kura 59.

MATUKIO MBALI MBALI KWENYE MKUTANO MKUU KATIKA PICHA





Saturday, July 11

HII HAPA TANO BORA YA CCM HII HAPA


Taarifa ambazo zimethibitishwa kupitia mtandao wa twitter wa CCM na mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete zinasema kuwa, Kamati Kuu ya CCM imekamilisha kazi na kuwapitisha wagombea watano.




Wagombea waliopitishwa ni Bernard Membe, January Makamba, Dkt Asha Rose Migiro, Dkt John Magufuli na Balozi Amina Salum.