KATIBU wa
uchumi na fedha wa chama cha usafirishaji Mkoani Iringa, Obedi Luhwago
ameamua kujitisa kuwania udiwani katika kata ya Luhota, jimbo la Kalenga
wilayani Iringa kwa tiketi ya Chama Cha Mapnduzi (CCM).
Akizungumza
na Uhuru, Mtove alisema kuwa ameamua kuwani nafasi hiyo ili aweze
kushirikiana na wananchi wa kata hiyo katika kuleta maendeleo.
Alisema
lengo lake ni kuhakikisha anasimamia kwa ufasaha utekelezaji wailani ya
CCM kwenye kata hiyo endapo, chama chake kitampa ridhaa ya kukimbiza
bendera kwenye kata hiyo.
“Nimeamua
kutangaza nia baada ya baraza la madiwani kuvunjwa kwa sababu tayari
filimbi imepiga kelele, ninayo nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa
kata ya Luhota,”alisema.
Luhwago
alisema angeweza kuwania kata ya mjini ambako hivi sasa anaishi, lakini
kutokana na mahitaji ya nyumbani kwao, ameamua kurejea kijijini, ili
aweze kuwania kata yao.
Aliwaomba
wananchi wa kata hiyo kumuunga mkono wakati utakapofika, kwa madai kuwa
kwa ushirikiano wao wanaweza kusogeza gurudumu la maendeleo.
Akizungumzia
upinzani, Luhwago alisema kuwa wananchi wanaimani kubwa na CCM kutokana
na utekelezaji wake wa ilani, katika kipindi kinachoisha.
“Viongozi
wanaomaliza muda wao wamefanya kazi na kuleta imani ya chama kwa
wananchi, kwa sababu hiyo CCM itaendelea kushika hatamu katika uchaguzi
ujao, na wapinzani hawataambulia chochote,” alisema.
Kumekuwa na wimbi kubwa na wana CCM kujitisa kwenye chaguzi mbalimbali jambo ambalo linaonyesha kukuwa kwa demokrasia.
No comments:
Post a Comment