Mashabiki
wa Arsenal wameamka asubuhi ya leo na kukutana na stori ambayo
inaihusisha klabu yao kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Karimu
Benzema.
Habari hiyo imeandikwa ukurasa wa nyuma wa gazeti la The Sun akisema kwamba Arsenal wapo tayari kulipa dau la paundi milioni 40.
The Sun wameongeza kwamba Arsene Wenger yuko tayari kulipa dau hilo mapema Jumatatu ijayo.
Je, Safari hii stori ni nini? kwanini tuamini kwamba Arsenal wanaweza kumsajili Benzema majira haya ya kiangazi?
Wiki
kadhaa zilizopita, Gazeti la AS la Hispania liliripoti kwamba kocha wa
Real Madrid, Rafa Benitez anataka kubadili mfumo wa uchezaji wa klabu
hiyo kuanzia msimu ujao.
Katika
ripoti hiyo ilielezwa kwamba msimu ujao Cristiano Ronaldo atacheza kama
mshambuliaji wa kati kwasababu Benitez anapendelea mfumo wa 4-2-3-1.
Zaidi, gazeti hilo lilisema kwamba Benzema mwenye umri wa miaka 27 hatapenda kucheza msimu ujao akianzia benchi.
Sasa
tetesi zimeenea kwamba Arsenal wameanza kuongea na viongozi wa Benzema
kuona uwezekano wa kumsajili na ndio maana gazeti la The Sun limekuja na
stori hiyo leo.
Hapa chini ni baadhi ya Tweets baada ya Arsenal kuhusishwa kumsajili Benzema;
No comments:
Post a Comment