Makocha
wa timu za Yanga na Gor Mahia ya Kenya wamezungumzia mchezo wao wa
kesho ambao ndio utakuwa mchezo wa ufunguzi kwenye michuano ya Kagame
Cup mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam
kuanzia majira ya saa 10:00 za jioni kwa saa za Afrika ya Mashariki.
Kila kocha ametamba kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuwa ni mkali kutokana na ubora wa vikosi vya timu zao.
Yanga
ndio mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara ambayo ilimalizika mwezi Mei
mwaka huu wakati wapinzani wao wakiwa wanaongoza ligi ya Kenya
inayoendelea kutimua vumbi nchini humo.
Kocha
wa mkuu wa Yanga Hans Van Pluijm amesema anawaheshimu sana wapinzani
wake timu ya Gor Mahia lakini hawaogopi na anamatumaini makubwa ya
kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.
“Nimekuwa
Afrika tangu mwaka 1996 hivyo ninauzoefu na soka la timu za hapa kwa
muda mrefu, tumefanya maandalizi ya kutosha kwa ajili ya kuikabili kila
timu kwenye michuano hii. Kitu kikubwa ni kwamba, mimi huwa sidharau
mpinzani wangu kwasababu kwenye soka lolote linaweza kutokea na hakuna
mtu anayejua matokeo”, amesema Pluijm.
Kwa
upande wake kocha mkuu wa Gor Mahia Mcotish Frank Nuttal amesema yeye
hana uzoefu mkubwa kwenye soka la Afrika ukilinganisha na mpinzani wake
(Van Pluijm) lakini akasisitiza kuwa vijana wake wako vizuri kuikabili
Yanga kesho kwenye uwanja wa Taifa.
“Yanga
ni timu kubwa japo sijawahi kuiona ikicheza lakini naamini ni timu
yenye ushindani na mechi ya kesho itakuwa ngumu lakini mwisho wa mchezo
tutajua matokeo”, amesema kocha huyo.
No comments:
Post a Comment