Friday, July 17

unajua chadema wamejipangaje ubunge na udiwani mwaka huu?

CHADEMA-LOGO 
 
Kuanzia jana July 15 hadi 19 mwaka huu 2015 CHADEMA wameanza rasmi utaratibu Wagombea wa Ubunge na Udiwani kuchukua na kurudisha fomu kwenye Majimbo yenye Wabunge wa chama hicho.
 
Baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza majimbo mapya 26 ya Uchaguzi, CHADEMA imelazimika pia kupangua ratiba ya awali na sasa kimeruhusu wanachama wote wenye sifa kuchukua na kurudisha fomu za kuwania uteuzi wa ndani ya chama katika nafasi za udiwani na Ubunge katika majimbo yote ya Uchaguzi nchi nzima.
 
Wagombea wa Udiwani wao ratiba iko tofauti kidogo, watachukua kurudisha fomu katika kata zote Tanzania kuanzia July 15 2015 hadi July 29 2015 saa 10 jioni.
 
“Wagombea ambao walishachukua na kurejesha fomu wana haki ya kuamua jimbo lipi wanaenda kugombea na hawalazimiki kuchukua fomu upya…watatakiwa kuujulisha uongozi wa chama ngazi ya jimbo kwa barua rasmi kuonesha kuwa fomu yake iwe ni ya jimbo lipi kati ya jimbo mama ama jipya na nakala ya barua hiyo inakiliwe ngazi ya wilaya, mkoa, kanda na taifa,” >>>> Katibu Mkuu Dk. Slaa.
 
Ratiba ya CHADEMA imeonesha kura ya maoni itaanza tarehe 20-25 July 2015 kwa kuzingatia Mwongozo wa Taratibu za Kura ya Maoni wa CHADEMA.

No comments: