Kuna baadhi ya watu wanaamini Tattoo
ni moja kati ya njia za utunzaji kumbukumbu za matukio muhimu
mwilini..na wakati mwingine hata kupamba mwili kwa mchoro wowote
anaovutiwa nao mtu.
Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko kubwa
kwa mastaa wa kitanzania kuchora tattoo mwilini mwao na wengine wengi
kutoka katika tasnia tofautitofauti.
Leo nimekuletea picha za mastaa nane wa soka duniani waliochora tattoo na maana zake
David Beckham
Huyu anatajwa kuwa ni miongoni mwa
wachezaji soka wenye mvuto duniani na mmoja kati ya sifa zake na uwezo
wake wa kipekee uwanjani ni kuwa na uwezo wa kupiga mipira iliyokufa
(faulo) na kufunga moja kwa moja, naye pia ni miongoni mwa mastaa wenye
michoro mwilini tattoo na ikiwa na maana tofauti tofauti…..Tattoo za Beckham
kuna zinazowakilisha mafanikio mbalimbali aliyoyapata katika
soka,michoro ya watoto wake na mahusiano yake ya kimapenzi na mke wake Victoria Beckham.
Zlatan Ibrahimovic
Ni raia wa Sweden, na
anapendwa sana nchini kwake kutokana na uwezo wake mkubwa wa kusakata
kabumbu kuna kipindi ziliwahi kuzuka tetesi kuwa kuna watu
wanaopendekeza picha yake iwe katika hela ya nchi hiyo (krona) lakini
sheria ikawa hairuhusu. Ni mkorofi lakini ni moja kati ya mastaa
wanaopenda kuchora michoro mwilini(tattoo) ana mchoro wa Red Dragon mgongoni kwake, Japanese Koi fish na “Only God Can Judge Me” ubavuni mwake.
Neymer da Silva Santos Junior
Ni nyota wa kibrazil ana chenga za
maudhi lakini ni moja kati ya wale mastaa wanaotumia mwili wao kama
Diary kwa kuchora kumbukumbu kwa michoro ya tattoo mwilini, ana tattoo
nyingi zenye misemo tofauti ya kireno zinazo mkumbusha furaha yake
wakati yuko mdogo, mchoro kama heshima kwa mtoto wake lakini pia
ameandika majina ya dada zake mwilini.
Dani Alves
Huyu ni beki asiye na maneno mengi hivyo
licha ya kutunza kumbukumbu kwa michoro ya tattoo mwilini mwake,
amekuwa akitumia mwili wake pia kutuma ujumbe kwa kuchora baadhi ya
michoro mwilini mwake, ana mchoro unaowakilisha imani yake ya kidini ya
kikatoliki, ameandika jina la mwanae kifuani mwake, mchoro wenye ujumbe
kwa familia yake, mchoro begani mwake wenye kumbukumbu ya mke wake wa
zamani Dina.
Kevin-Prince Boateng
Huyu ni ndugu wa damu na Jerome Boateng ambaye anaichezea timu ya taifa ya Ujerumani huku Kevin akiichezea Ghana waliamua kugawanyika kwa mapenzi yao wenyewe, Kevin aliamua kuchezea taifa la baba yake Ghana na Jerome aliamua kuchezea taifa la mama yake Ujerumani. Licha ya kuzaliwa na kukulia Ujerumani Kevin ameonyesha mapenzi yake ya dhati kwa Afrika kama muafrika aliyezaliwa na kukulia Afrika kwa kuchora ramani ya Afrika katika mkono wake wa kulia na nchi yake ya Ghana ana mchoro pia wa klabu ya Ac Milan, mchoro wa Spider na kumbukumbu ya jeraha lake la goti.
Lionel Messi
Huyu huwa anatajwa kama Diego Maradona wa kizazi hiki hasa ukizingatia wanasifa zinazoshabiana kiuchezaji, kasi na wote wanatumia miguu ya kushoto…. Messi
pia ana michoro mingi ya tattoo ila mmoja uliokuwa katika headlines
sana ni pale alipochora viganja vya mikono na jina la mtoto wake Thiago kwenye mguu wake wa kushoto, lakini pia ana tattoo ya picha ya Yesu kwenye mkono wake wa kulia juu karibu na bega.
Marcelo da Silva Junior
Unakumbuka timu ya taifa ya Tanzania iliwahi kwenda kuweka kambi Brazil? basi zile hostel walizofikia Brazil aliwahi kuishi zamani beki wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil Marcelo
ambaye inadaiwa aliwahi kukata tamaa ya kupata mafanikio katika soka na
alitaka kuachana na soka kabla babu yake kumtia moyo na kumsii
kutofanya hivyo. Marcelo ana
michoro mingi ya tattoo kwa kuiona tu huwezi jua maana yake ila ana
tattoo anayo ithamini kumbukumbu ya babu yake mtu ambaye angeweza
kufanya Marcelo leo hii dunia isimtambue katika soka kama tu angeunga mkono kukata tamaa kwa Marcelo.
Thiery Henry
Ni mchezaji aliyetamba na Arsenal
kwa takribani miaka tisa anatajwa kuwa mfungaji bora wa muda wote wa
klabu hiyo… Ana tattoo nyingi tu hususani mikononi ila huwa hazionekani
mara kwa mara kwa sababu ya tabia yake ya kupenda kuvaa jezi za mikono
mirefu. Moja ya tattoo hizo ni ya picha ya binti yake Tea Henry aliyoichora kwenye mkono wake wa kushoto.
No comments:
Post a Comment