Mama wa Iker Casillas ameamua kuomba radhi kwa kauli yake ya kwamba mwanaye anapaswa kuchezea timu bora zaidi ya Porto.
Kwa
pamoja, Mari Carmen Fernandez na mumewe, Jose Luis, walibaki na msimamo
wao kwamba mtoto wao alikuwa hapati heshima anayostahili katika klabu
yake ya Real Madrid, ambayo Jumamosi aliaga rasmi kutimka klabuni hapo
kuelekea maskani yake mpya katika klabiu ya Porto.
Mama
wa Casillas alienda mbali zaidi kwa kuwafananisha wababe hao wa Dragao
katika timu za daraja la tatu lakini ameamua kuomba radhi kwa tukio
hilo.
"Pengine sikuwa sahihi", alikaririwa na gazeti la Marca.
"Nataka
kuwashukuru Porto kwa kumsajili mwanangu.
Natumaini watafanya kazi bega
kwa bega ili kuipa mafanikio klabu.
Ningependa mnisamehe mara 1,000.
Natumaini mwanangu atapata mafanikio kama alivyopata akiwa Madrid.
"Iker
alifanya majaribio yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 8. Mara zote
alikuwa akijitoa asilimia zote kwa ajili ya klabu.
Siku zote amekuwa ni
mwenye nidhamu na heshima kubwa.
"Nadhani
mashabiki wamekuwa ni watu wema sana kwa mwanangu.
Nimekuwa
nikishuhudia, kwa moyo mkunjufu mashabiki wakimshangilia mwanangu pindi
atokapo uwanjani".
No comments:
Post a Comment