Meneja
wa Manchester United, Louis van Gaal amethibitisha kwamba bado
anahitaji kusajili wachezaji wawili majira haya ya kiangazi licha ya
ukweli kuwa ameshanasa saini ya wachezaji wanne mpaka sasa.
Van
Gaal ametumia paundi milioni 80 kumsajili winga wa PSV Eindhoven,
Memphis Depay, beki wa kulia wa Torino, Matteo Darmian na viungo Bastian
Schweinsteiger kutoka Bayern na Morgan Schneiderlin Southampton.
Mholanzi huyo ameiambia MUTV kuwa bado ana mapengo mawili katika kikosi chake.
"Hapana,
hatujamaliza usajili". Amesema Van Gaal na kuongeza: " Tutanunua
mchezaji ambaye anaweza kuleta mchango, nadhani bado tunahitaji kuongeza
wachezaji wawili katika sehemu mbili na tutafanya hivyo pale
inapowezekana".
Van
Gaal pia anamuwinda mlinzi wa kati Sergio Ramos, lakini dau la paundi
milioni 40 alilotuma Real Madrid limekataliwa mara kadhaa, wakati huo
inaelezwa kwamba Man United wanataka kumuuza Jonny Evans.
Van Gaal amesema kwamba Javier Hernandez "Chicharito" atakuwa sehemu ya kikosi chake.
No comments:
Post a Comment