Monday, July 13

STERLING RASMI NI MANCHESTER CITY



Hatimaye klabu za Liverpool na Manchester City zimefikia makubaliano katika sakata la usajili wa kiungo mshambuliaji wa Liverpool, Raheem Sterling na kutua City kwa ada ya uhamisho wa pauni 49m.
Sakata hili lililoteka hisia za mashabiki duniani kote ikiwa ni pamoja na vyombo vya habari, limefikia tamati wakati ambao timu zinajiandaa na msimu mpya.
 
Katika makubaliano baina ya vilabu hivyo vya uingereza, Manchester City watalipa pauni 45m kwanza na kisha kuongeza pauni 4m kutokana na ushiriki wa Raheem katika kikosi hicho za Manchester.
 
Liverpool walikataa ofa ya kumuuza mchezaji huyu kwenda City zaidi ya mara mbili huku wakikomaa kupata pauni 50m kwa kijana huyu mwingereza mwenye asili ya Jamaica.
 
Sterling ambae majuma kadhaa yaliyopita alitajwa kama mmoja wa wanandinga wenye thamani zaidi chipukizi, amewachukiza sana mashabiki wa Liverpool ambao wanamuona dogo huyo kuwa mkosa adabu na heshima kwa klabu.
 
Aidha nahodha aliyeondoka kikosini hapo dirisha hili, Steven Gerrard amekaririwa akimlaumu mchezaji huyo kwa kukosa subira ya mafanikio ndani ya Liverpool na kuhofia kwamba litakua si jambo jema kwa Raheem kukaa benchi Manchester City wakati anapata nafasi kikosi cha kwanza, akiwa na Liverpool

No comments: