Serikali ya Somalia leo hii
itafungua rasmi kesi dhidi ya kenya katika Mahakama ya kimataifa (ICJ)
kufuatia mgogoro wa mpaka baina ya nchi hizo mbili.
Somalia inailamu kenya kuwa inamiliki sehemu ya bahari kwa njia isiyo halali.
Mgogoro huu umekuwa ukiendelea kwa miaka sita sasa.
Somalia inaipeleka Kenya katika mahakama ya kimataifa huko The Hague Uholanzi kwa madai kwamba kenya imekataa usuluhishi nje ya mahakama.
Somalia na Kenya zinagombea sehemu ya bahari kwa madai kuna mafuta na gesi katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment