Tuesday, September 22

NAFASI 368 ZA KAZI ZIMEPIGANIWA NA WAOMBAJI MIL.2.3 NCHINI INDIA....

>>ni nafasi za ulinzi na uhudumu wa chai maofisini

>>maafisa wa serikaliwasema iwapo watafanyiwa intervie mmoja mmoja, itamalizika mwaka 2020,

>>wao wakili maisha nchini india ni magumu kutokana na uhaba wa ajira


Wakati nchi ya india ikitajwa kuwa ifikapo mwaka 2030 itaongoza kuwa na idadi kubwa ya watu baada ya takwimu za hivi sasa kuonesha kuwa nchi ya China ndio inayoshika nafasi ya kwanza kwa kuwa na Idadi kubwa ya watu Duniani ikiwa na jumla ya watu Bilioni 1.38, nafasi ya pili ni India ambayo ina jumla ya watu Bilioni 1.31, kati ya idadi ya Dunia nzima ya watu Bilioni 7 !!


lakini licha ya hayo pia ikumbukwe kuwa tatizo la ukosefu wa ajira ni tatizo kubwa sana sasa hivi kila sehemu Duniani, hivyo hivi karibuni Serikali ya India ilitangaza nafasi 368 za kazi kwa Walinzi pamoja na Wahudumu wa Chai Maofisini, lakini unaambiwa kwenye nafasi hizo hizo 368 watu waliojitokeza kuomba nafasi walikuwa watu Milioni 2.3.

Maofisa wa Serikali wamesema kama kila mtu aliyetuma maombi ya kazi akiitwa kwenye Interview maana yake ni kwamba itachukua miaka minne mpaka kuwapata watu watakao ajiriwa kwenye nafasi hizo.

Wengi walioomba kazi wanasema walipoona tangazo ilibidi watume maombi kwa sababu hakuna ajira na maisha ni magumu.

Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa, UN zinaonesha mpaka kufikia mwaka 2030 India itaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu, ikifuatiwa na China na Marekani.

 India Thing

No comments: