Tuesday, February 16

JIPU..TBC..

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amewasimamisha kazi watumishi wawili wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kutokana na utendaji usioridhisha.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TBC Dar es Salaam jana, Nape aliwataja watumishi waliosimamishwa kazi kuwa ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Matukio, Mbwilo Kitujime na Meneja wa Vipindi, Edna Rajab ambao wamesimamishwa kazi na uamuzi huo utafikishwa kwa Bodi ya TBC kwa hatua zaidi.“Tunachukua uamuzi wa kuwasimamisha kazi watendaji hawa ili kujenga upya Idara hii muhimu katika ustawi wa TBC na habari kwa ujumla,” alisema Nape.
Aidha, Waziri huyo amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TBC kuwachukulia hatua watumishi wengine walio chini ya Idara hiyo kwa kuwa wako chini ya mamlaka yake na kutoa mrejesho wa hatua alizochukua dhidi ya wale wote wilioonesha utendaji mbovu.

No comments: