Nitahakikisha nakupatia kila stori
inayonifikia….sasa hivi nakusogezea hii stori kutoka shirika la Umeme
Tanzania (Tanesco) kuhusu kuwasimamisha kazi maofisa 7 waandamizi
kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo wizi na ubadhirifu.
Akizungumza leo Dec 6, 2015 mbele ya waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba alisema…’Ukiacha
kero zinazosababisha na Miundombinu TANESCO inachukua hatua madhubuti
za kuwaadhibisha wafanyakazi wake wanaotoa huduma mbaya na kuwa kero kwa
wateja baadhi ya kero ambazo zimekuwa zikilalamikiwa pamoja na lugha
mbaya, wateja kudaiwa rushwa kabla ya kupewa huduma kucheleweshewa
huduma, ubadhirifu‘ – Mramba
‘Shirika linapenda kuwahakikishia
wateja wake kuwa tayari limeanza kuchukua hatua kali kwa wafanyakazi
wanaobainika kujihusisha na mambo hayo’ – Mramba
Kwa mfano
katika kipindi cha miezi miwili Shirika limewaachisha kazi maofisa 7
waandamizi kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo wizi na
ubadhirifu.Miongoni mwao ni wale waliofikishwa mahakamani kule Kagera
na kuripotiwa na vyombo vya habari jana.Walioachishwa kazi ni pamoja na
wafanyakazi wa ngazi za Mameneja, wahandisi na wahasibu’ – Mramba
‘Shirika
litaimarisha hatua hizo ambapo mfanyakazi yeyote atakayebainika
analaghai wateja, anadai rushwa anatoa lugha chafu au huduma mbovu
atawajibishwa mara moja na pale atakapobainika kuachishwa kazi‘Mramba
No comments:
Post a Comment