Kampuni
wa usafiri inayofanya safari zake kati ya Ufaransa na Uingereza ya
Eurotunnel imesema maelfu ya wahamiaji wamekuwa wakijaribu kuingia
nchini Uingereza kupitia usafiri huo.
Ripoti ya kampuni hiyo
imebainisha kuwa idadi ya majaribio ya wahamiaji kutaka kuvuka mpaka
kupitia usafiri aina hiyo ya usafiri imeongezeka mno,kwani wahamiaji hao
watu hao wanajificha kwenye magari ya mizigo,kupanda vizuizi ilimradi
tu waingine katika vyombo hivyo vya usafiri na kuvuka.Katika mkutano wa Mawaziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa na Uingereza uliofanyika mjini London,mbinu za pamoja kuweza kudhibiti wahamiaji hao kuvuka zimejadiliwa na kuelezea hali kuwa ni tatizo kubwa kwa sasa.
Wahamiaji hao kutoka nchi za Sudani na Afghanstan waliopo bandari ya Calais nchini ufaransa ya Calais ndiyo waliobainika kutaka kuvuka kwenda nchini Uingereza kwa mfumo huo, wengi wa wahamiaji hao wanatoka nchini Sudan na Afghanstan.
Mwaziri hao wa mambo ya ndani wa Ufaransa na Uingereza wanasema wamebaliana tutafanya kazi pamoja kuwarejesha wahamiaji hawa ambao wengi wao wanatoka Afrika Magharibi,na kuwahakikishia watu kwamba safari za aina hii haziwi lango kuu la wahamiaji kuingia Uingereza.
Na tayari serikali ya Ufaransa imekwisha anza kuweza jitihada za ziada kama idadi zaidi ya askari,na uingereza itatoa kiasi cha paundi million saba kuimarisha ulinzi,japo kuwa Mbunge wa Bunge la Ulaya Claude Moraes anasema haamini kama hatua ya kuwarejesha wahamiaji hao makwao kutasaidia kutatua tatizo hilo
No comments:
Post a Comment