Wednesday, July 29

WATOTO ZAIDI YA LAKI NANE WA WAWA WAKIMBIZI KUTOKANA NA BOKO HARAM

http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/f2a9424294eab82a94b0322b732579f0_XL.jpg 
Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa(Unicef) umeeleza wasiwasi wake kuhusu kuendelea hujuma za kundi la Boko Haram zilizosababisha mamia ya maelfu ya watoto nchini Nigeria kuwa wakimbizi.


Unicef imetangaza kuwa mashambulizi na jinai zilizofanywa na kundi la wanamgambo wa Boko Haram katika miaka ya hivi karibuni zimewafanya watoto wa Nigeria zaidi ya laki nane kuwa wakimbizi; huku wengi wa watoto wao wakilazimishwa kuolewa au kuwa watumwa wa ngono.


Takwimu mpya za Unicef zinaonyesha kuwa, idadi ya watoto waliolazimika kuwa wakimbizi kutokana na mashambulizi ya Boko Haram imeongezeka mara mbili mwaka uliopita. 


Wakimbizi wengi kutoka Nigeria huelekea katika nchi jirani za Chad, Cameroon na Niger, ambazo ni miongoni mwa nchi maskini zaidi duniani, huku raia hao wakiwa na suhula chache za kujikimu na maisha na kujilinda.

No comments: