Monday, November 30

WAMETUAGA HAWAAA....KWAHERI KOBE BRYANT, KWAHERI BLACK MAMBA,KWAHERI ROLE MODEL WA VIJANA WENGI WAPENDA BASKET, KWAHERI MTU WA KIKAPU... NI MUDA ULIFIKA SASA, NA SISI WOTE TUPO NYUMA YAKO. AHSANTE KWA YOTE ULIYOTUFANYA TUNAYAONE NDANI NA NJE YA UWANJA.....

kobbKobe Bryant , ambaye alisaidia Lakers kushinda mataji  matano ya NBA baada ya kuwa katika NBA kwa zaidi ya miaka  20 ambayo yote ameichezea timu aloipenda daima ya Los Angeles Lakers.
Kobe alitangaza Jumapili kwenye tovuti ya Wachezaji ‘kwamba ameamua kustaafu baada ya msimu huu , huku akiandika kwamba ” msimu huu ndio pekee uliobakia kwangu wa kuwapa nilichonacho. ”
Kobe aliandika kwa mtindo wa shairi huku akiliita “Dear Basketball” na ndani yake kukiwa na maneno kadhaa ya kugusa moyo wa kila mpenda michezo.
kobe
Mojawapo ni kauli ya “huu ndio mchezo uliompa   na kumtizimia ndoto mtoto aliyekuwa na umri wa mika 6 (akimaanisha mtotoyeye) tu ya kuchezea Lakers na nitaupenda kwa hilo siku zote.”
” Lakini siwezi kukupenda kwa dhati ile kwa muda mrefu, ” Bryant aliandika. ” Msimu huu ndicho ambacho mimi nimebakiwa nacho ambacho naweza kutoa. Moyo wangu unaweza kabisa kukabiliana na vurugu .
Mawazo yangu yanaweza vyema kushughulikia misuguano  lakini mwili wangu unajua ni wakati wa kusema kwaheri. “Na hiyo ni sawa . Mimi niko tayari ili uondoke uende zako mmpenzi basketball . ”
barua ya Kobe kuhusu kustaafu waliyokuwa wanagawiwa mashabiki mlangoni katika mchezo dhidi ya Pacers
barua ya Kobe kuhusu kustaafu waliyokuwa wanagawiwa mashabiki mlangoni katika mchezo dhidi ya Pacers
Kocha wa Lakers Bryon Scott alisisitiza kuwa Kobe Bryant atacheza mchezo wa Jumapili ambayo itakuwa jumatatu alfajiri kwa Afrika Mashariki. Katika taarifa yake Scott alisema ni kweli kuwa Bryant atastaafu lakini sio kwamba hatocheza maana amesema kuwa ni msimu wake wa mwisho na ataucheza kwa nguvu zote ikiwezekana.
“Nadhani yeye bado anaupenda sana mchezo huu ,” Scott aliwaambia waandishi wa habari . “Kiukweli  bado ana shauku kubwa kwa ajili yake na kikubwa  bado ni kijana mwenye ushindani wa hali a juu.
kobe
” Scott alisema alikuwa ” alistushwa ” wakati Bryant anampa taarifa yake Jumamosi usiku kwamba alikuwa anaenda kutangaza kustaafu kwake siku inayofuata.
kobee
“Alinistua aliponiletea taarifa hiyo kiasi fulani,” Scott alisema. Pengine nitakuwa mtu ninayesikitika kwa hili kuliko mtu yoyote mwingine au kitu chochote kile. Mtu ambaye nina mapenzi makubwa sana kwake na mtu ambaye nimekuwa nikiheshimu sana uwezo wake.
Siku zote huwa ni vigumu sana mtu wa kariba ya Kobe katika mchezo akiamua kutundika kila kitu” Hata hivyo mara kadhaa Kobe alikuwa akinukuliwa kwa kuelezea kuwa alifikiri huu ungeweza kuwa msimu wake wa mwisho.
Na kwa kuzingatia namna alivyoanza msimu kwa kiwango kibovu sio jambo geni sana lakini kwa rekodi, uwezo na jina alilojijengea katika NBA ni wazi kuwa ni taarifa kubwa sana.
Kobe Bryant ameshinda kila kitu katika NBA. Akicheza kwa miongo miwili yaani miaka 20, ameshinda tuzo ya MVP, kashinda mmedali zadhahabu za Olympic, kashiriki NBA All Star mara 17, ameshinda ubingwa wa NBA mara sita, kashinda tuzo za MVP za All star.
Hakuna alichobakisha au pointi zake 81 alizofunga katika mchezo mmoja. Pia ni mchezaji wa tatu aliyefunga pointi nyingi zaidi katika NBA.
koben
Kamishna wa Ligi kuu  ya kikapuMarekani, Adam Silver naye alitoa maoni yake kwa kusema awe anagombea ubingwa wa NBA, au akiwa katika uwanja tupu wa mazoezi akijaribu kurusha mitupo yake, Kobe Bryant anabaki kuwa mchezaji na mtu mwenye Upendo mkubwa kwa mchezo huu.

PATA HII...BALE, RONALDO KILA MMOJA ATUPIA MADRID IKIITANDIKA EIBAR 2-0 NYUMBAN......


Eibar: Riesgo, Capa, Pantic, Dos Santos, Junca, Escalante, Dani Garcia, Adrian (Verdi 69 mins), Saul Berjon, Inui, Enrich (Arruabarrena 86)
Subs not used: Irureta, Ramis, Silvestre, Harjovic, Luna
Booked: Dos Santos, Escalante

Real Madrid: Navas, Carvajal (Benzema 85), Nacho, Pepe, Danilo, Kroos, Modric, Kovacic (Casemiro 79), Rodriguez (Lucas Vazquez 65), Bale, Ronaldo
Subs not used: Casilla, Arbeloa, Cheryshev, Lazo
Goal: Bale 43, Ronaldo pen 82











MTAZAMO WA SALEH ALLY....KUHUSU JEZI ZA KILIMANJARO STARS..........

KILA siku binadamu anajifunza jambo jipya, huenda jana halikuwepo au kusikika. Lakini leo mambo yanabadilika na linakuwa gumzo au linalotakiwa kufanyiwa kazi.

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ndiyo ulizaa Tanzania yenye Bara na Visiwani. Hili ni jambo ambalo Watanzania wengi wamekuwa wakilipigania kuhakikisha linadumu.
Lakini kuna kitu ambacho nilikifikiria, lakini pia nikapata changamoto kutoka kwa mdau mmoja wa soka. Linahusu jezi ambazo timu zetu tatu kubwa za taifa zimekuwa zikitumia.
Tuna Taifa Stars ambayo inajumuisha Tanzania Bara na Visiwani na hii ndiyo inayobeba picha ya muungano hasa.
Taifa Stars inatuwakilisha kila tunapokwenda kushiriki mashindano yoyote chini ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) na lile la Afrika (Caf).
Lakini tuna timu nyingine mbili ambazo zinakuwa wawakilishi wa Watanzania wakati wa michuano ua Ukanda wa Afrika Mashariki. Hiyo ni michuano ya Chalenji ambayo Bara wanawakilishwa na Kilimanjaro Stars huku Visiwani wakiwakilishwa na Zanzibar Heroes.
Hizi timu zinakuwa zinajitegemea kwa maana ya ukanda na Tanzania inakuwa na wawakilishi kutoka pande mbili. Jambo ambalo ni zuri kwa kuwa linatanua wigo zaidi.
Sitaki kuingia kwenye ile vita ya Zanzibar nao wamekuwa wakitaka uwakilishi upande wa Caf na Fifa. Mimi zaidi nitalenga kwa upande wa jezi, bora zikiwa za aina tatu tofauti na sasa ni aina mbili.
Wachezaji wa Zanzibar wanapokuwa pamoja wale wa Tanzania Bara, wanaunda Taifa Stars na kutumia jezi moja. Wakienda kwenye michuano ya Chalenji, Zanzibar Heroes wanakuwa na jezi zao lakini Kilimanjaro Stars wanabaki na jezi za Taifa Stars.
Hii kidogo ndiyo inanipa mkanganyiko, ndiyo maana nikaamua kuifikisha hapa kama sehemu ya mjadala. Simlaumu mtu, badala yake natamani nanyi mlifikirie hili ana kuona nini kifanyike.

Binafsi ninaona itakuwa sahihi kama kutakuwa na jezi za aina tatu tofauti. Kwa kuwa tayari zipo za Taifa Stars na Zanzibar Heroes, basi Kilimanjaro Stars ingekuwa na jezi zake zinazojitegemea kabisa.

Kwangu naona hii, kwanza italeta usawa sahihi na maana sahihi ya kuwa Tanzania ina timu tatu tofauti zenye hadhi ya kuitwa timu ya taifa. Lakini itatengeneza taswira inayoeleweka kwa kila kikosi kati ya hivyo vitatu.
Kwa sasa taswira ya kikosi cha Kilimanjaro Stars, imejificha ndani ya kivuli cha Taifa Stars, jambo ambalo ninaona si sahihi hata kidogo, kwa nia nzuri tu.

Tuaiacha Taifa Stars iendelee kujitegemea kuliko kuifanya Kilimanjaro Stars ni sawa na Taifa Stars wakati inakuwa haina wachezaji kutoka Zanzibar.

Tuwafanye wachezaji wapate hisia ya tofauti kati ya Taifa Stars na Kilimanjaro Stars kama ambavyo wanavyoipata wale wanaokwenda Zanzibar Heroes, kwa kuwa jezi pekee zinaweza kuwapa hisia hiyo, sasa wako upande upi.
Hili si kosa, huenda watu hawakuwahi kuliona kama ni muhimu sana lakini kwangu naona lina umuhimu mkubwa kuanzia kwa maana, kwenda kwa wachezaji wenyewe kwa hisia lakini pia hata thamani pia hisia za mashabiki.
Ninaamini bado wachezaji wanapaswa kujua heshima ya jezi hizo tatu. Pia bado wana kila sababu ya kujua, kufanya vizuri katika klabu, kufanya vizuri zaidi katika Zanzibar Heroes na Kilimanjaro Stars ni uhakika wa kuitumikia Taifa Stars ambayo inatubeba Watanzania wote.
Jezi haliwezi kuwa jambo gumu sana kama TFF itaamua kulifanyia kazi mara moja na kulimaliza hilo. Baada ya hapo, utambuzi na tofauti zitakuwa wazi.
Hakuna haja ya kuepuka au kuona si sahihi kwani hata majina tu ya timu zenyewe, yanaonyesha jezi zinatakiwa kuwa tatu tofauti.

Kila la kheri Kilimanjaro Stars katika michuano ya Chalenji dhidi ya Ethiopia, leo.

Vichwa vya Habari za Magazeti ya Tanzania... November 30 2015 na stori zake kubwa kurasa za mwanzo na mwisho.......


Leo  November 30 2015 nimekuwekea tena stori zote kubwa za Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye Udaku, michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea Mtanzani Mwenzangu....
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC02882
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Viongozi kujadili athari za joto duniani....



Mazungumzo kuhusu Mabadiliko ya tabia nchi yanaanza rasmi asubuhi ya leo huko jijini Paris nchini ufaransa, wakuu wa nchi zaidi ya mia na hamsini wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo uliondaliwa na umoja wa mataifa.
Maandamano yamefanayika duniani kote kushinikiza kuchukuliwa hatua kupambana na ongezeko la joto duniani, jijini Paris Polisi walilazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwasambaratisha waandamanaji huku watu mia moja wakishikiliwa kwa kosa la kukiuka amri ya kutofanya maandamano iliyotolewa baada ya mashambulizi jijini humo.
Akifungua mkutano huo, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius, alisema ana uhakika kuwa mazungumzo hayo yatawafikisha kwenye hatua ya makubaliano chanya.
Wakati huo huo rais Obama amezuru kituo cha burudani cha Bataclan mjini Paris kutoa heshima zake kwa waathiriwa na shambulio la kigaidi wiki mbili zilizopita. Obama na rais wa nchi hiyo, Francois Hollande waliweka shada la maua kwenye ukumbi huo, ambako watu tisini waliuawa na wanamgambo wa Kiislamu waliokuwa wamejihami kwa bunduki.