Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam
imetoa maamuzi ya kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na kada wa Chadema
aliyekuwa akiiomba mahakama hiyo kutoa uamuzi wa kwamba wananchi
wanatakiwa kukaa mita ngapi baada ya kupiga kura.
Mahakama hiyo imelitolea suala hilo ufafanuzi na kusema kuwa ni
marufuku kwa wananchi kukusanyika katika kituo cha kupigia kura na hata
njee ya mita 200 hairuhusiwi kwani ni kinyume cha sheria.
Kesi hiyo namba 37 ya mwaka huu, ilifunguliwa na mgombea ubunge wa Viti
Maalum kwa tiketi ya Chadema, Amy Kibatala, dhidi ya Mwanasheria Mkuu
wa Serikali (AG) na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(Nec) chini ya hati ya kiapo cha dharura.
Oktoba 16, mwaka huu, mlalamikaji alifungua kesi ya kikatiba iliyopewa
usajili namba 37, ya mwaka huu akiiomba Mahakama itoe tafsiri ya kifungu
cha 104 kidogo cha (1) cha Sheria ya Uchaguzi kama kinazuia ama
kuwaruhusu wananchi kukaa kwa utulivu umbali wa mita 200, baada ya
kupiga kura katika vituo.
No comments:
Post a Comment