Mgeni
Rasmi, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Prof. Adolf Mkenda
akihutubia wadau mbalimbali wa takwimu katika maaadhimisho ya Siku ya
Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa
na kauli mbiu ya “Takwimu Bora kwa Maisha Bora”.
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo ya
utangulizi katika katika maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika
yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu
ya “Takwimu Bora kwa Maisha Bora”
Mkuu
wa Kitengo cha Teknolojia, Habari na Mawasiliano Dkt. Carina Wangwe
kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii
(SSRA) akielezea umuhimu wa kujiunga katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii
wakati wa maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo
Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya “Takwimu Bora
kwa Maisha Bora”.
Mkuu
wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Prof. Innocent Ngalinda
akielezea umuhimu wa takwimu rasmi katika kupanga na kutathmini programu
mbalimbali za maendeleo nchini wakati wa maaadhimisho ya Siku ya
Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa
na kauli mbiu ya “Takwimu Bora kwa Maisha Bora”.
SOMA ZAIDI »
Tuesday, November 24
KUHUSU RAIS WA ZANZIBAR....MGOGORO WA ZANZIBAR WATUA IKULU YA MAREKANI......
Wakati vikao vya siri vya kutafuta suluhu ya mzozo wa kisiasa visiwani Zanzibar vikiwa vimeripotiwa, juhudi za kuupatia ufumbuzi mzozo huo zimehamia kutoka Ikulu ya Zanzibar na kufika Ikulu ya Marekani (White House).

Mnamo tarehe 21 mwezi huu, Wazanzibari waishio nchini Marekani waliandamana hadi kwenye Ikulu ya nchi hiyo katika juhudi za kutafuta uingiliaji kati wa kimataifa ili kuupatia suluhisho mzozo huo.
Akizungumza na waandishi wa habari mbele ya Ikulu hiyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari Waishio nchni Marekani (ZADIA) iliyoandaa maandamano hayo Bwana Omar Haji Ali, alisema kuwa maandamano hayo yanakuja katika juhudi za Jumuiya hiyo za kutafuta uingiliaji kati wa kimataifa katika kuukwamua mgando wa kisisas visiwani Zanzibar.
Aliendelea kusema kwamba maandamno hayo pia yana lengo la kumkumbusha rais Barack Obama wa Marekani kutekeleza ahadi yake ya kuilinda demokrasia Barani Afrika. "Katika hotuba yake aliyoitoa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika mapema mwaka huu, rais Obama alisema '.. pale ambapo raia hawawezi kutekeleza haki zao, basi ulimwengu una jukumu la kukemea. Na Marekani itafanya hivyo, hata kama wakati mwengine itakuwa inauma'..", alikumbusha Bwana Ali.
Aliongeza kuwa "Wananchi wa Zanzibar wameshindwa kutekeleza haki yao kwa zaidi ya nusu karne sasa. Wakati umefika sasa kwa ulimwengu kuchukua jukumu lake. Wakati umefika sasa kwa Marekani siyo tu kukemea, lakini pia kuchukua hatua za kivitendo ili kuhakikisha kuwa sauti za Wazanzibari zinasikilizwa na kuheshimiwa"
Alipoulizwa ni hatua gani watakazochukuwa iwapo Serikali ya Marekani haikuchukua hatua yoyote kusaidia kumaliza mgando wa kisiasa Zanzibar, Bwana Ali alisema "Tuna imani na rais Obama, na tumemfikishia barua ya malalamiko yetu, na tunasubiri jibu lake, na imani yetu ni kuwa atachukua hatua madhubuti khususan ikizingatiwa kuwa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ulikuwa wa mwanzo kutoa taarifa kuelezea kuwa uchaguzi wa Zanzibar ulikuwa wa haki na huru" Alidokeza kuwa, iwapo hali itaendelea kubakia kama ilivyo, basi ZADIA itaelekea kwnye Umoja wa Mataifa.

Katika maandamano hayo yaliyowashirikisha pia wapenda amani na demokrasia kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni, waandamanaji walibeba mabango yaliyokuwa na maneno kama vile "Mshindi wa uchaguzi atangazwe", "maamuzi ya Wazanzibari yaheshimiwe", "bila haki hakuna amani' na mengineyo.
Aidha, waandamanaji hao walipiga makelele wakidai "tunataka matokeo yetu ya uchaguzi.."
Akizungumza na Swahilivilla, raia mmoja wa Marekani aliyeshiriki kwenye maandamano hayo alisema "Nilimpeleka mwanangu kwenda kusoma kule, bado ana mapenzi na Zanzibar, na amenisimulia habari nzuri za amani, utulivu na ukarimu wa watu wake. Amekuwa akifuatilia hali ilivyo, na kwa hamasa kubwa alipopata habari za maandamano haya, akaniomba tuje kuwaunga mkono Wazanzibari katika kudai haki yao"
Itakumbukwa kuwa, wananchi wa Zanzibar walipiga kura mnamo tarehe 25 Oktoba mwaka huu, lakini Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Bwana Jecha Salum Jecha akatangaza kufutwa kwa uchaguzi huo Mkuu visiwani humo, kitendo ambacho wataalamu wa Sheria wamesema kuwa kinakwenda kinyume na Katiba ya Zanzibar.
Wachambuzi wanaona kuwa hatua hiyo ya Bwana Jecha ilikuja wakati asilimia kubwa ya matokeo yaliyokuwa yametangazwa yalikuwa yanampa ushindi mgombea wa urais wa Zanzibar kutoka chama cha upinzani cha Wananchi (CUF) Maliim Seif Shariff Hamad.
Kitendo cha kufutwa kwa uchaguzi huo ambao wachunguzi wa nje na ndani waliulezea kuwa ulikuwa wa haki na huru, kimezua mtafaruku wa kisiasa visiwani Zanzibar, na juhudi za ndani na nje zimekuwa zikifanyika ili kumaliza mgogoro wa kisiasa visiwani humo.
Maandamano ya ZADIA ni katika juhudi za hivi karibuni kabisa za kimataifa za kusaka suluhu za mgogoro huo kwa njia za amani.

Mpenda amani na Demokrasia Lodi Mohamed akiongea na muandishi wa habari Njee ya Ikulu ya Marekani (White House)
UNDP YAKABIDHI MRADI WA DOLA ZA MAREKANI 150,000 WA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI KIJIJI CHA CHAMWINO....
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja waMataifa la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), kijijini humo. Bango la mradi uliozinduliwa na Bw. Alvaro Rodriguez.
Mfaham Huyu Hapa...Msanii wa bongofleva aliethibitisha kupata Zero kwenye mtihani wa Form IV...
Kwenye muziki wa bongofleva tunae Nuh Mziwanda ambaye pia ni boyfriend wa msanii Shilole…… Nuh ameongea ukweli wa moyoni kwenye exclusive interview na millardayo.com na kusema >>> ‘Kwenye maisha yangu ninachojutia ni nilivyofeli mtihani wangu wa form IV nilipata Zero kabisa na sikufanya mitihani kama mitatu, yote hiyo ilitokea sababu ya muziki’
‘Nilikua mtoto mwenye akili sana na Mama yangu alikua anategemea nitakuja kuwa mtu flani mwenye elimu yake kwenye familia yetu na sio Mwanamuziki, nyumbani kwetu tuko watano na mimi ndio wa mwisho na nilikua nina akili sana kuliko wote na kuanzia la kwanza mpaka la saba nilikua sishuki kwenye Wanafunzi kumi bora‘ – Nuh
Nuh amesema kuna uwezekano wa kurudi shule >>> ‘shule ni kitu muhimu haikataliwi, ni kitu poa unakuwa Mwanamuziki alafu una elimu yako… na muziki naudai sana ndio maana naukazania sababu ulinifanya nifeli shule’
Soma Vichwa Vya Habari kubwa za Magazeti 14 ya Tanzania leo... November 24 2015 kwenye Udaku, michezo na hardnews.....
Leo November 24 2015 nimekuwekea
tena stori zote kubwa za Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye Udaku,
michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea Duniani...
Sunday, November 22
Algeria kumshitaki kocha wa Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa...Hizi sababu zao....
November 17 timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ilicheza mchezo wake wa pili wa kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 Urusi dhidi ya timu ya taifa ya Algeria mjini Blida katika uwanja wa Mustapha Tchaker, ikiwa ni siku tatu tu zimepita toka wacheze mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu michuano hiyo uwanja wa Taifa Dar Es Salaam na kumalizika kwa sare ya goli 2-2.
Mchezo wa pili uliyochezwa mjini Blida ulimalizika kwa Algeria kuibuka na ushindi wa goli 7-0 ila kabla ya mchezo huo kuanza waalgeria wana mtuhumu Mkwasa kutoa kauli za kibaguzi, hivyo wamepanga kumshitaki kwa shirikisho la mpira wa miguu ulimwenguni FIFA kwa kusema wao ni wabaguzi wa rangi.
Full Kilichotokea....Burundi Vs Zanzibar Heroes CECAFA Challenge 2015 …
Michuano ya Kombe la mataifa ya Afrika Mashariki na kati maarufu kama CECAFA Senior Challenge Cup yameanza leo November 21 mjini Addis Ababa Ethiopia, ikiwa ni michezo miwili ilikuwa inatarajia kuchezwa leo November 21, timu ya Zanzibar Heroes dhidi ya timu ya taifa ya Burundi ndio zilikuwa timu za kwanza kufungua dimba kabla ya wenyeji Ethiopia watakaocheza dhidi ya Rwanda.
Burundi ambao walikuwa na nyota wao kadhaa akiwemo Didier Kavumbagu anayekipiga katika klabu ya Azam FC ya Tanzania walikuwa wakiutawala mchezo kwa wastani kumiliki mpira kwa asilimia 56 katika kipindi cha kwanza wakati Zanzibar walikuwa na asilimia 44 za umiliki wa mpira kwa dakika zote 45 za kwanza.
Mchezo huo ambao Burundi walikuwa wakifika sana langoni kwa Zanzibar Heroes hadi wanaenda mapumziko walikuwa wanaongoza kwa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Didier Kavumbagu dakika ya 38. Licha ya kipindi cha pili Zanzibar kutafuta nafasi ya kusawazisha goli hilo haikuwezekana.
Kuna mita 200 nyingine....Uchaguzi mkuu leo Nov 22?? Upate Ukweli Uliopo....
Kwa mujibu wa tume ya taifa ya uchaguzi NEC uchaguzi wa nafasi ya mbunge katika jimbo husika utalazimika kurudiwa endapo mmoja kati ya wagombea atafariki kabla ya uchaguzi kufanyika.
Hapa kaimu mkurugezi wa NEC Bw. Emmanuel Kawishe ametoa ratiba nzima na taratibu za kufuata kwa wapiga kura wote>>>
“Vituo vitafunguliwa saa 1 kamili asubuhi na kufungwa saa 10 kamili za jioni, iwapo wakati wa kufunga kituo kukawa na watu waliokatika foleni na walifika kabla ya saa 10 watapata nafasi ya kupiga kura”
Baada ya kupiga kura taratibu gani itafuata? Kalieleza na hili>>
“Matokeo yote yakishapokelewa na msimamizi wa uchaguzi yatajumlishwa mbele ya mawakala na watu wote wanaoruhusiwa, baada ya kuhesabu kura fomu zitatiwa saini na mawakala watakaokuwepo.”
Rais Magufuli tena.. ni baada ya lile agizo kutoka kwenye hafla ya Wabunge....
Katibu mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema fedha hizo zimefanikisha kupatikana vitanda 300 vya wagonjwa pamoja na magodoro yake, shuka 600, baiskeli za kubebea Wagonjwa na vifaa vingine na kwamba hivyo vyote tayari vimepelekwa katika hospitali ya taifa Muhimbili.
Balozi Sefue ameuagiza uongozi wa Hospitali hiyo kuhakikisha vitanda vyote vimefungwa Jumapili ya November 22 2015 na kisha Rais mwenyewe atakwenda Hospitalini hapo Jumatatu ya November 23 2015 viwe vyote vimefungwa tayari vinatumiwa na wagonjwa waliokosa vitanda.
Wadau mbalimbali walichangia kiasi cha shilingi milioni mia mbili ishirini na tano (225) kwa ajili ya kugharamia hafla ya Wabunge baada ya uzinduzi wa bunge la kumi na moja Dodoma lakini Rais Magufuli aliagiza fedha hizo zitumiwe kwa kiasi kidogo kisichozidi shilingi milioni 15 na nyingine zipelekwe hospitali ya Muhimbili kutatua tatizo la uhaba wa vitanda.
Subscribe to:
Posts (Atom)

