Friday, November 20
MKALI WA ACTION MOVIE....Pichaz 8 za mkali wa movie kutoka Hollywood Van Damme alivyotembelea mazoezi ya Man City.....
Staa wa movie kutoka Hollywood Jean-Claude Van Damme mkali ambaye amewahi kutamba na movie kadhaa November 19 alipata nafasi ya kutembelea mazoezi ya klabu ya Manchester City. Staa huyo wa Hollywood yupo jijini Manchester kwa ajili ya shughuli ya ‘black-tie dinner’ ambapo atapata nafasi ya kuoneshwa kwa movie zake.
Jean-Claude Van Damme ambaye ana umri wa miaka 55 alivyotembelea mazoezi ya Man City mastaa wa klabu hiyo hawakuacha kuchukua kumbukumbu zao kwa kupiga picha na staa huyo, wachezaji wa Man City kama Yaya Toure, Vincent Kompany, Kevin De Bruyne, Sergio Aguero pamoja na kocha wao Manuel Pellegrini hawakusita kupiga picha na Van Damme.
Mkali huyo wa movie duniani ambaye kwa
miaka ya karibuni ametamba katika tangazo la bia, amewahi kutamba katika
movie za mapigano zikiwemo Bloodsport, Hard Target na Universal Soldier. Hizi ni baadhi ya pichaz zake alivyotembelea Man City.
Thursday, November 19
MSHUHUDIE KILICHOMTOKEA...Mchungaji kawalisha waumini nyoka na nguo za ndani!!!..
Hizi stori kutoka kwa viongozi wa nyumba
za ibada kuwa na matendo yanayoibua maswali mengi sio ngeni masikioni
mwetu, nimeinasa nyingine toka South Africa, Mchungaji kawalisha Waumini
wake nyoka pamoja na nguo za ndani..
Mchungaji huyo Penuel Mnguni ambaye ni Kiongozi wa Kanisa la End Times Disciples Ministries lililopo katika Mji wa Soshanguve ulioko Pretoria South Africa,
alijikuta akiishia mikononi mwa watu wenye hasira na matendo yake, huku
Kanisa lake likiteketea baada ya kuchomwa moto na watu haohao !!
Taarifa zilienea mitaani kuhusu huduma
zake, alikuwa akiwalazimisha waumini wake kula nyoka pamoja na nguo za
ndani kama sehemu ya huduma za Kanisa lake kwa Waumini… watu wa eneo
hilo waliwavamia na kumkamata Mchungaji huyo, Kanisa likaishia kuchomwa
moto, ambapo baada ya muda kidogo ilibidi Polisi waingilie kati
kumuokoa.
HUYU HAPA NDIYO WAZIRI MKUU WA TANZANIA KUTOKA BUNGENI..2015....
BREAKING
NEWS: Mh. Kassim Majaliwa Mbunge wa Ruangwa amependekezwa na Rais John
Magufuli kuwa Waziri Mkuu mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Waziri Mkuu aliyependekezwa Mh. Kassim Majaliwa ni mbunge kupitia jimbo la Ruangwa na ana umri wa miaka 54.
Waziri Mkuu aliyependekezwa Mh. Kassim Majaliwa ni mbunge kupitia jimbo la Ruangwa na ana umri wa miaka 54.
TAIFA STARS..Kichapo cha Bao 7-0 kwa Taifa Stars dhidi ya Algeria kimemvunjia rekodi hii Mkwasa …
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars November 17 ilicheza mchezo wake wa pili wa marudiano ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2018 Urusi dhidi ya Algeria Blida katika uwanja wa Mustapha Tchaker na kukubali kipigo cha magoli 7-0, idadi ya magoli ambayo iliifanya Tanzania kuingia katika headlines ya ya kufungwa idadi kubwa ya magoli.
November 18 kocha wa timu hiyo Charles Boniface Mkwasa
ameongelea namna alivyokipokea kipigo hicho na kufanya kiweke historia
kwake kwani kwa miaka yake 25 katika soka hakuwahi kuweka rekodi ya
kupokea kipigo cha magoli mengi kiasi hicho kitu ambacho hakikuwaumiza
watanzania hata yeye.
“Kiukweli
hata mimi ilinishangaza kidogo na tulizidiwa umeona uwezo wa mchezaji
wao Yacine Brahimi uwezo wake ni mkubwa kikosi chao kilibadilika ila
uwanja pia ulikuwa tatizo ulikuwa unateleza hata goli la kwanza
tulilofungwa lilitokana na hivyo, kufungwa goli 7 sijawahi kiukweli
katika miaka 25 yangu katika soka” >>> Boniface Mkwasa
Wednesday, November 18
Rapa Mkali Toka Kitambo..Snoop Dogg aponda vikali orodha ya Billboard ya rappers wakali wa muda wote....
Rapa mkongwe duniani Snoop Dog ameponda vikali orodha
ya rapa wakali zaidi wa muda wote iliyotolewa na tovuti ya Billboard
wiki iliyopita.
Majina kwenye orodha hii yalikuwa pamoja na Biggie,
Jay Z, Eminem, Rakim, Nas, Andre 3000, Lauryn Hill, Ghostface Killah,
Kendrick Lamar na Lil Wayne.
Snoop Dogg amekasirishwa kuwa Tupac hakutajwa kwenye orodha hii. Haya ndio maneno yake kwenye instagram >>“This is so disrespectful. !!“Whoever did this list need a swift kick in the Ass. No. Tupac. Come on cuz ?. Jus my opinion.“
Subscribe to:
Posts (Atom)
