Monday, November 30

MTAZAMO WA SALEH ALLY....KUHUSU JEZI ZA KILIMANJARO STARS..........

KILA siku binadamu anajifunza jambo jipya, huenda jana halikuwepo au kusikika. Lakini leo mambo yanabadilika na linakuwa gumzo au linalotakiwa kufanyiwa kazi.

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ndiyo ulizaa Tanzania yenye Bara na Visiwani. Hili ni jambo ambalo Watanzania wengi wamekuwa wakilipigania kuhakikisha linadumu.
Lakini kuna kitu ambacho nilikifikiria, lakini pia nikapata changamoto kutoka kwa mdau mmoja wa soka. Linahusu jezi ambazo timu zetu tatu kubwa za taifa zimekuwa zikitumia.
Tuna Taifa Stars ambayo inajumuisha Tanzania Bara na Visiwani na hii ndiyo inayobeba picha ya muungano hasa.
Taifa Stars inatuwakilisha kila tunapokwenda kushiriki mashindano yoyote chini ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) na lile la Afrika (Caf).
Lakini tuna timu nyingine mbili ambazo zinakuwa wawakilishi wa Watanzania wakati wa michuano ua Ukanda wa Afrika Mashariki. Hiyo ni michuano ya Chalenji ambayo Bara wanawakilishwa na Kilimanjaro Stars huku Visiwani wakiwakilishwa na Zanzibar Heroes.
Hizi timu zinakuwa zinajitegemea kwa maana ya ukanda na Tanzania inakuwa na wawakilishi kutoka pande mbili. Jambo ambalo ni zuri kwa kuwa linatanua wigo zaidi.
Sitaki kuingia kwenye ile vita ya Zanzibar nao wamekuwa wakitaka uwakilishi upande wa Caf na Fifa. Mimi zaidi nitalenga kwa upande wa jezi, bora zikiwa za aina tatu tofauti na sasa ni aina mbili.
Wachezaji wa Zanzibar wanapokuwa pamoja wale wa Tanzania Bara, wanaunda Taifa Stars na kutumia jezi moja. Wakienda kwenye michuano ya Chalenji, Zanzibar Heroes wanakuwa na jezi zao lakini Kilimanjaro Stars wanabaki na jezi za Taifa Stars.
Hii kidogo ndiyo inanipa mkanganyiko, ndiyo maana nikaamua kuifikisha hapa kama sehemu ya mjadala. Simlaumu mtu, badala yake natamani nanyi mlifikirie hili ana kuona nini kifanyike.

Binafsi ninaona itakuwa sahihi kama kutakuwa na jezi za aina tatu tofauti. Kwa kuwa tayari zipo za Taifa Stars na Zanzibar Heroes, basi Kilimanjaro Stars ingekuwa na jezi zake zinazojitegemea kabisa.

Kwangu naona hii, kwanza italeta usawa sahihi na maana sahihi ya kuwa Tanzania ina timu tatu tofauti zenye hadhi ya kuitwa timu ya taifa. Lakini itatengeneza taswira inayoeleweka kwa kila kikosi kati ya hivyo vitatu.
Kwa sasa taswira ya kikosi cha Kilimanjaro Stars, imejificha ndani ya kivuli cha Taifa Stars, jambo ambalo ninaona si sahihi hata kidogo, kwa nia nzuri tu.

Tuaiacha Taifa Stars iendelee kujitegemea kuliko kuifanya Kilimanjaro Stars ni sawa na Taifa Stars wakati inakuwa haina wachezaji kutoka Zanzibar.

Tuwafanye wachezaji wapate hisia ya tofauti kati ya Taifa Stars na Kilimanjaro Stars kama ambavyo wanavyoipata wale wanaokwenda Zanzibar Heroes, kwa kuwa jezi pekee zinaweza kuwapa hisia hiyo, sasa wako upande upi.
Hili si kosa, huenda watu hawakuwahi kuliona kama ni muhimu sana lakini kwangu naona lina umuhimu mkubwa kuanzia kwa maana, kwenda kwa wachezaji wenyewe kwa hisia lakini pia hata thamani pia hisia za mashabiki.
Ninaamini bado wachezaji wanapaswa kujua heshima ya jezi hizo tatu. Pia bado wana kila sababu ya kujua, kufanya vizuri katika klabu, kufanya vizuri zaidi katika Zanzibar Heroes na Kilimanjaro Stars ni uhakika wa kuitumikia Taifa Stars ambayo inatubeba Watanzania wote.
Jezi haliwezi kuwa jambo gumu sana kama TFF itaamua kulifanyia kazi mara moja na kulimaliza hilo. Baada ya hapo, utambuzi na tofauti zitakuwa wazi.
Hakuna haja ya kuepuka au kuona si sahihi kwani hata majina tu ya timu zenyewe, yanaonyesha jezi zinatakiwa kuwa tatu tofauti.

Kila la kheri Kilimanjaro Stars katika michuano ya Chalenji dhidi ya Ethiopia, leo.

Vichwa vya Habari za Magazeti ya Tanzania... November 30 2015 na stori zake kubwa kurasa za mwanzo na mwisho.......


Leo  November 30 2015 nimekuwekea tena stori zote kubwa za Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye Udaku, michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea Mtanzani Mwenzangu....
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
DSC02882
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

Viongozi kujadili athari za joto duniani....



Mazungumzo kuhusu Mabadiliko ya tabia nchi yanaanza rasmi asubuhi ya leo huko jijini Paris nchini ufaransa, wakuu wa nchi zaidi ya mia na hamsini wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo uliondaliwa na umoja wa mataifa.
Maandamano yamefanayika duniani kote kushinikiza kuchukuliwa hatua kupambana na ongezeko la joto duniani, jijini Paris Polisi walilazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwasambaratisha waandamanaji huku watu mia moja wakishikiliwa kwa kosa la kukiuka amri ya kutofanya maandamano iliyotolewa baada ya mashambulizi jijini humo.
Akifungua mkutano huo, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius, alisema ana uhakika kuwa mazungumzo hayo yatawafikisha kwenye hatua ya makubaliano chanya.
Wakati huo huo rais Obama amezuru kituo cha burudani cha Bataclan mjini Paris kutoa heshima zake kwa waathiriwa na shambulio la kigaidi wiki mbili zilizopita. Obama na rais wa nchi hiyo, Francois Hollande waliweka shada la maua kwenye ukumbi huo, ambako watu tisini waliuawa na wanamgambo wa Kiislamu waliokuwa wamejihami kwa bunduki.

Tuesday, November 24

USINDI SURA MBAYA...SHINDANO LA SURA MBAYA ZIMBABWE LAMALIZIKA KWA GHASIA.....

Ghasia zimeibuka baada ya mwanaume mwenye umri wa miaka 42 kutangazwa kuwa mshindi katika shindano la mtu mwenye sura mbaya Jijini Harare nchini Zimbabwe, huku mashabiki wakiwatuhumu majaji kwa upendeleo.

Majaji hao walimchagua, Mison Sere, kuwa mshindi kutokana na kutokuwa na meno mengi na kuwa na uwezo wa kuibadilisha sura yake kwa kuikunja kunja, na kumshinda bingwa mtetezi William Masvinu, ambaye amekuwa bingwa tangu mwaka 2012.

Mshindi wa shindano la mwanaume mwenye sura mbaya nchini Zimbabwe, huibuka na zawadi ya dola 500, ambayo ni fedha nyingi ukizingatia wengi wa washiriki wa shindano hilo huwa hawana ajira maalum.
                                      Washiriki wa sura mbaya wakiwa katika mapozi tofauti 
                    Mshindi wa shindano la sura mbaya Mison Sere akiwa amebebwa juu

ZIARA YA HAPA KAZI TU...KATIBU MKUU KIONGOZI OMBENI SEFUE AFANYA ZIARA MUHIMBILI...

SEF1
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akisisitiza jambo katika mkutano na waandishi wa habari ambao umefanyika leo katika ukumbi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kuhusu utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli kwamba wagonjwa hawapaswi kulala chini. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru. Picha zote kwa hisani ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
SEF2
Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue akisaini kitabu cha wageni mara baada baada yakwasili hospitalini hapo.
SEF3
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (katikati) akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ambako amefanya ziara kuangalia utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli kuhusu huduma bora kwa wagonjwa na kutekeleza wagonjwa kutolala chini. Wagonjwa hivi sasa wanalala kwenye vitanda na siyo chini. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi na Jamii, Dk Donan Mmbando na kulia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa ya Moi, Othuman Wanin Kiloloma.
SEF4
Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue akihoji kutokamilika kwa mashine ya MRI kwa wakati baada ya kutembelea chumba ambako mashine hiyo imehifadhiwa. Ofisa anayesimamia utengenezaji wa mashine hiyo, Monica ameahidi kwamba mashine hiyo itakamilika Alhamisi ijayo.
SEF5
Mmoja wa mafundi wa mshine ya ST-Scan akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Kiongozi (kulia), Balozi Ombeni Sefue kuhusu utengenezaji wa mashine hizo. Fundi huyo ameahidi kwamba mashine hiyo itakamilika Jumatano.
Picha zote kwa hisani Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue leo amefanya ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) pamoja na mambo mengine amesema serikali itaendelea kuboresha sekta ya afya nchini ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati.
 
Akizungumza baada ya kutembelea MNH, Balozi Sefue amesema amekagua mashine za MRI na CT-SCAN na kueleza kuwa spea zimeshafika na kazi ya kutengeneza mashine hizo inaendelea. 
 
Pia amesema kwamba Serikali ya Tanzania imesaini mkataba mpya na Serikali ya Uholanzi wa kununua vifaa vipya na Hospitali ya Muhimbili itapata CT-SCAN moja wakati Hospitali ya Bugando itapata mashine moja ya MRI.
 
Pia, amewataka wahudumu wa afya kuwahudumia vizuri wagonjwa wanaotumia Bima ya Afya ili kuongeza mapato katika hospitali za serikali.
Akizungumzia kuhusu kudhibiti wizi wa dawa za serikali, Balozi Sefue amesema ni vema ukaimarishwa mfumo wa MSD kwa kutumia mifumo ya 
 Tehama na kuwa na maduka yao ya ndani.
 
Katika ziara hiyo, Balozi Sefue amepata fursa ya kufanya kikao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dk Donan Mmbando na watendaji wa MNH ili kupata sura ya matatizo yote katika hospitali hiyo.

HATIMA YA MWILI WA MAREHEMU MAWAZO KUAGWA JIJINI MWANZA KUAMULIWA LEO NA MAHAKAMA.....


                                          

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema leo kimefungua kesi katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, ili kuiomba Mahakama hiyo kutengua zuio la kuuaga mwili wa aliekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Geita Marehemu Alphonce Mawazo, lililotolewa na Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kutokana na hofu ya kiusalama pamoja na uwepo wa ugonjwa wa Kipindupindu.

Katika kesi hiyo, Chadema inawakilishwa na Mawakili watatu ambao ni James Millya, John Mallya pamoja na Paul Kipeja ambapo mlalamikaji ni Charles Lugiko ambae ni baba mdogo wa Marehemu Mawazo.

Mahamaka hiyo chini ya Jaji Lameck Mlacha, imesikiliza malalamiko ya upande wa washtaki na kuahirisha kesi hiyo hadi kesho ambapo imeamuru mlalamikiwa ambae ni Mkuu wa Polisi Mkoa wa Mwanza pamoja na mwanasheria Mkuu wa Serikali kupelekewa nyaraka za kesi hiyo kabla ya kusikiliza utetezi wao hapo kesho.

Mapema kabla ya kesi hiyo kusikilizwa, wafuasi wa Chadema waliokuwa wamekusanyika nje ya viunga vya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, walilalamikia hatua ya jeshi la polisi kuwazuia kuingia Mahakamani hapo ili kujua hatima ya kesi hiyo, ambapo wamesema kitendo hicho kinaondoa dhana ya Rais John Pombe Magufuli, kuwa yeye ni rais wa wananchi wote wakati wao kama Chadema wananyimwa haki zao.

Licha ya Malalamiko hayo pamoja na ulinzi mkali wa polisi uliokuwa umetanda Mahakamani hapo, bado wafuasi wa Chadema hawakuondoka katika viunga vya Mahakama hiyo hadi pale Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Freeman Mbowe alipowasihi kurejea majumbani mwao hadi kesho kesi hiyo itakaposikilizwa tena.

Ni zaidi ya siku nane sasa tangu marehemu Alphonce Mawazo auawe kikatili Mkoani Geita na watu wasiojulikana kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni chuki za kisiasa ambapo mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando.
SOMA ZAIDI »

BALOZI SEFUE AWAASA WATUMISHI WA UMMA KUWAJIBIKA.....

OM1 
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Bw Silasi David mmoja ya wagonjwa waliolazwa katika kitengo cha mifupa cha MOI.
OM2
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na mmoja ya wagomjwa waliolazwa katika kitengo cha mifupa cha MOI Bw. Muhusin Hamiri. 

                                                                                 Na Beatrice Lyimo- Maelezo
Watumishi wa umma wametakiwa kutumia muda wa kazi kuhudumia wananchi na sio kufanya kazi zao binafsi kwa kutumia ofisi na vifaa vya serikali.
Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alipofanya ziara katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kwa lengo la kuangalia maendeleo ya Hospitali kwa kukagua vifaa tiba na kuongea na watendaji wakuu wa hospitali hiyo.
Balozi Sefue ameongeza kuwa watumishi wa umma wanapaswa kufanya kazi kwa kutoa huduma bora na kwa upendo kwa wananchi kwani moja ya kanuni na taratibu za mtumishi wa umma ni kumhudumia mteja pasipo upendeleo.
 

“kwa upande wa madaktari na watoa huduma za afya mnatakiwa kutoa huduma bora na  zenye upendo kwa wananchi ili nao wajione wanahaki ya kupatiwa huduma hiyo”.
 

“kwa watumishi wote wa umma tukijitambua kuwa sisi ni watumishi wa umma tutafanya kazi kwa bidii na kwa kujituma” alifafanua Balozi Sefue.
Pia muda wa kuingia na wa kutoka ofisini na pia kujipima ni nini amefanya ndani ya masaa nane katika kuhudumia wananchi.
 

“Hizi si nguvu za soda ni lazima kubadilika pindi tunapowahudumia wateja kwa wakati na kwa ufanisi” alisema Balozi Sefue.
adhalika katika kuhakikisha serikali inatoa huduma bora kwa wananchi Balozi sefue ameagiza katika kila ofisi itoayo huduma kuwe na dawati la msaada kwa wananchi waweze kupata huduma kwa haraka.

MAADHIMISHO YA SIKU YA TAKWIMU AFRIKA YAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM......

T1
Mgeni Rasmi, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Prof. Adolf Mkenda akihutubia wadau mbalimbali wa takwimu katika maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya “Takwimu Bora kwa Maisha Bora”.
T2
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo ya utangulizi katika katika maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya “Takwimu Bora kwa Maisha Bora”
T3
Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia, Habari na Mawasiliano Dkt. Carina Wangwe kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) akielezea umuhimu wa kujiunga katika Mifuko ya Hifadhi za Jamii wakati wa maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya “Takwimu Bora kwa Maisha Bora”.
T4
Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Prof. Innocent Ngalinda akielezea umuhimu wa takwimu rasmi katika kupanga na kutathmini programu mbalimbali za maendeleo nchini wakati wa maaadhimisho ya Siku ya Takwimu Afrika yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambayo yameongozwa na kauli mbiu ya “Takwimu Bora kwa Maisha Bora”.
SOMA ZAIDI »