Ni masaa machachetu tangu kusambaa kwa ujumbe ulioandikwa kupitia Instagram account ya staa wa bongo fleva Belle 9 ikionyesha kumdiss staa mwenzake bongoflevani Diamond Platnumz,
Mgombea
wa Democratic Hillary Clinton na mgombea wa Republican Donald Trump
wamechukua uongozi wa mapema katika mchujo wa kuteua wagombea urais
Marekani katika vyama vyao.
Mahakama
ya hakimu mkazi Singida imewahukumu washitakiwa sita adhabu ya kutumikia
jela jumla ya miaka 120 na kulipa faini ya jumla ya zaidi ya shilingi
Bilioni 1.4, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumiliki kinyume na
sheria vipande 53 vya tembo vyenye thamani ya shilingi 149,336,000 na
kosa la jingine la uwindaji.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix
Ngamlagosi (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
Dar es Salaam jana, kuhusu bei kikomo za mafuta aina ya petroli kuanzia
leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Umeme, Mhandisi Anastas Mbawala.
BAADHI
ya wazazi wa wanafaunziwaliokuwa wakisoma Chuo Kikuu cha St Joseph
katika matawi ya Arusha na Songea wametupa lawama kwa Tume ya vyuo
vikuu nchini (TCU) kwa hatua yake ya kufuta vibali vya kuanzisha matawi
hayo na kwamba hali hiyo imewathiri watoto wao.
March 2 2016 naanza kwa kukusogezea post
ya stori zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia
kwenye , Michezo na hardnews ili ujue kinachoendelea
Huenda ukawa umezoea na kuboreka na foleni ya jiji la Dar Es Salaam ambalo wakati mwingine inaweza kukugharimu kwa zaidi ya saa moja kukaa katika foleni kutoka Tegeta hadi Posta, hususani mvua ikiwa inanyesha Dar Es Salaam sehemu huwa zinakuwa na foleni kubwa. Mtu wangu wa nguvu nimekutana na list ya mpya kutoka www.telegraph.co.ukya miji 10 inayoongoza kwa foleni Duniani, imeandikwa 04/02/2016.
February 26 2016 naanza kwa kukusogezea post ya stori zote kubwa
zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye , Michezo na
hardnews ili ujue kinachoendelea....
Ikulu imeahidi kufanyia kazi madai ya Chama cha Wasanii Wachoraji
Tanzania (Chawata), ambayo waliyawasilisha jana, kikilalamikia ofisi
hiyo katika awamu ya nne iliyokuwa chini ya Rais Jakaya Kikwete,
kuwachelewa malipo yao ya Sh. milioni 53.6.
Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli, imeamua kutumia
mfumo wa ‘Cash Budget (kutumia kilichokusanywa), huku baadhi ya wachumi
wakisema utaleta nidhamu ya matumizi ya serikali na kubana watumishi
ambao walizoea kutumia vibaya fedha za umma kwa kuzipangia matumizi
yasiyo na tija. Wizara ya Fedha na Mipango imeeleza kuwa, mfumo wa
kupanga na kutumia kinachokusanywa na Mamlaka ya Mapato (TRA), ndiyo
ulioamuliwa kutumiwa na serikali ya awamu ya tano.Itakumbukwa kuwa,
tangu Novemba mwaka jana, mapato ya TRA yalipanda kutoka wastani wa Sh.
bilioni 800 na Sh. bilioni 900 kwa mwezi mpaka Sh. trilioni 1.3,
Desemba, mwaka jana Sh. trilioni 1.4, Januari, mwaka huu Sh. trilioni
1.06 na malengo ya Februari ni kukusanya Sh. 1.03. Jana Ofisa Habari
wa Wizara ya Fedha na Mipango, Ingiaheddi Mduma, alisema utaratibu wa
kutumia kilichokusanywa utaendelea kutumika kila mwezi. Alisema kila makusanyo yatakayopatikana kwa mwezi husika, yatatumika kulingana na mahitaji husika ya mwezi huo.
“ Mahitaji yakiwa mengi katika mwezi husika, basi hata fedha
itakayokusanywa kwa mwezi huo itatumika kulingana na mahitaji hayo,
tutakuwa tunafanya hivyo kila mwezi,” alisema Mduma.
Tanzania imedhihirisha kuwa ni tajiri mkubwa wa rasilimali ya gesi
asilia baada ya kugundulika kwa gesi nyingine katika bonde la mto Ruvu
yenye ukubwa wa ujazo wa futi trilioni 2.17. Ugunduzi huo wa gesi
asilia umefanywa na Kampuni ya Dodsal Hydrocarbons and Power Tanzania
Limited ambayo imekuwa inafanya shughuli za utafutaji wa gesi na mafuta
katika Mkoa wa Pwani.Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Pilavullathil
Surendran alisema jana katika mkutano wa wawekezaji wa gesi na mafuta
ulioandaliwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
kuwa, thamani ya gesi iliyoko katika eneo hilo inafikia Dola za Marekani
bilioni sita sawa na Sh trilioni 12. Ugunduzi huo mpya unafanya hadi sasa Tanzania kuwa na amana ya gesi yenye ukubwa wa futi za ujazo trilioni 57.27.
February 24 2016 naanza kwa kukusogezea post ya stori zote kubwa
zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye , Michezo na
hardnews ili ujue kinachoendelea....
February 21 2016 naanza kwa kukusogezea post ya stori zote kubwa zilizobebwa kwenye Magazeti ya Tanzania kuanzia kwenye , Michezo na haerdnews ili uju kinachoendelea......