Thursday, September 24

WAJUE MARAIS WALIOONGOZA KWA MUDA MREFU BARANI AFRIKA, YUPO MSEVEN NA DOS SANTOS



Suala la iwapo marais wanafaa kuruhusiwa kuwania kwa muhula wa tatu katika nchi ambazo katiba inasema kiongozi anafaa kuwa mamlakani kwa mihula miwili pekee limechipuka tena huko Congo-Brazzaville.

Rais wa taifa hilo Denis Sassou Nguesso ametangaza kuwa taifa hilo litaanda kura ya maamuzi kuamua iwapo ataruhusiwa kuwania kwa muhula wa tatu.

Mjadala sawa unaendelea nchini Rwanda.

Lakini je, wajua ni viongozi gani wa sasa wameongoza mataifa yao kwa muda mrefu zaidi Afrika?

Hawa hapa:

•Miaka 36: Teodoro Obiang Nguema Mbasogo - Equatorial Guinea, alichukua madaraka kupitia mapinduzi ya serikali mwaka Agosti 1979

• Miaka 36: Jose Eduardo dos Santos - Angola, alichukua uongozi baada ya kifo cha rais wa kwanza wa taifa hilo Agostinho Neto Septemba 1979

Miaka 35: Robert Mugabe - Zimbabwe, alishinda uchaguzi wakati wa kujinyakulia uhuru kwa taifa hilo Aprili 1980

• Miaka 32: Paul Biya - Cameroon, alichukua uongozi baada ya kujiuzulu kwa rais wa kwanza wa nchi hiyo Ahmadou Ahidjo, Novemba 1982

• Miaka 30: Denis Sassou Nguesso - Congo, aliwekwa uongozini na jeshi mwezi Oktoba 1979 na akaongoza hadi mwezi Agosti 1992. Alirejea tena Oktoba 1997 na kuendelea hadi sasa.

Miaka 29: Yoweri Museveni - Uganda, alichukua uongozi rais baada ya kundi lake la waasi kuchukua madaraka mwezi Januari 1986
BOFYA HAPA CHINI UONE MAFURIKO YA HATARI YA MGOMBEA

MANARA: YANGA HAWATAZUNGUMZA MILELEBAADA YA MECHI JUMAMOSI


MANARA
Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema uongozi wa Yanga hautapata nafasi ya kuzungumza kabisa.

KATIKA HALI ISIYOKUWA YA KAWAIDA MTARO WA KUPITISHIA MAJI MACHAFU HASA WAKATI WA MVUA UNAKARIBIA KUZIBWA NA MAGANDA YA MIWA YANAYOMWAGWA NA WAFANYA BIASHARA WA MIWA WALIOPO SOKO LA MIEMBENI MJINI DODOMA


KISA MAISHA WAKAAZI WA DODOMA WANAHATARISHA MAISHA YAO DAMPO




Wednesday, September 23

HABARI KUTOKA RASI FM RADIO..SEPT 23 MCHANA



picha na Maabara
DODOMA                     

Waumini wa dini ya kiislamu duniani kote wanatarajia kusherehekea sikukuu ya Eid El Hajj hapo kesho ambapo kwa mkoa wa Dodoma ibada ya pamoja  ya sikukuu ya swala ya eid el hajj I itakuwa katika uwanja wa jamhuri.

RAIS WA LA LIGA ATHIBITISHA KUWA FC BARCELONA MASHAKANI LA LIGA MUDA WOWOTE ITAONDELEWA....UNDANI UKO HAPA


Rais wa Ligi Kuu Hispania (LALIGA) Javier Tebas na waziri wa michezo wa Hispania  Miguel Cardenal wamethibitisha kama Catalonia ikijitenga na kutoka katika umoja wa Hispania klabu ya FC Barcelona ambayo inatokea Catalonia haitashiriki Ligi Kuu Hispania.

ULIYAPATA MATOKEO YA JANA SEPT 22 KATI YA SUNDERLAND DHIDI YA MANCHESTER UNITED? CHEKI HAPA NA HIGHLIGHTS ZOTE ZA MAGOLI


Klabu ya Manchester City usiku wa September 22 ilikaribishwa na klabu ya Sunderland katika uwanja wa Stadium of Light kucheza mchezo wa Kombe la Capital One, mechi imemalizika kwa klabu ya Manchester City kuibuka na ushindi wa goli 4-1.

Baada ya majibu ya TWAWEZA kuipa CCM ushindi wa 66 %, kwa ufupi sana Lowassa kajibu haya pia yupo zitto kabwe,January makamba lakini magufuli JP hajasema chochote


Kuelekea uchaguzi mkuu October 25 2015 matokeo ya utafiti wa taasisi ya TWAWEZA yametolewa September 22 2015 Tanzania na kuonyesha Watanzania mbalimbali wanamkubali nani zaidi ambapo CCM imepata 66%, CHADEMA ikipata 22%, C.U.F 1%, ACT 0%, NCCR 0%, UKAWA 3%.

ALIKIBA AFUNGUKA JUU YA RAIS AJAYE ANAYEMKUBALI, MCHEKI HAPA RAIS WAKE YEYE 2015


Ali K 5 

Wakati tukishuhudia wasanii kama kalla jeremiah, jack line wolper,Roma mkatoliki na wengineo wakiwa na mwelekeo wa kumshabikia mgombea urais kupitia ukawa yaani Edward Lowassa, huku pia JB,Aunty Ezekiel, Ray, Bi mwenda na wengineo nao wakimuunga mkono mgombea urais kupitia CCM John Pombe Magufuli, sasa rasmi msanii Ali Kiba nae amejiunga rasmi na kina Ray kumpa nguvu magufuli.

Hizi ndizo kurasa za mbele na nyuma za magazeti 17 ya kitanzania ya leoseptember 23 2015 ..




September 23 2015 ninazo tayari stori kubwakubwa kwenye kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania >>> Udaku, Hardnews na Michezo.
Jumla ya Magazeti 17 ya Tanzania tayari yamenifikia leo, nimekusogezea uzipate kurasa zake za mbele na za nyuma zilizobeba stori kubwa kwa leo.
DSC00626
DSC00627

Unajua kuwa imemchukua dakika 9 pekee Robert Lewandowski kufunga magoli matano katiuka mechi ya bayern munich dhidi ya Wolfsburg usiku wa jana? tazama magoli yote hapa {Videoz} 2015

Tuesday, September 22

RASI FM HABARI SAA 7:00 USIKU SEPT 22



Bukola SarakiDAR  ES  SALAAM                

Chama cha Wazazi wa Watoto Wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, Akili na Viungo (Chawaumavita) kimewataka wakina baba kuacha tabia ya uoga ya kukimbia majukumu pindi wanapopata watoto wenye ulemavu.

TAARIFA YA HABARI RASI FM RADIO SEPTEMBER 22.2015



KITAIFA:,
TANGA                                  
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan amevuna wanachama 272 Mkoani Tanga kutoka vyama mbalimbali vya upinzani baada ya wanachama wa vyama hivyo kujiunga rasmi na CCM.

Bi. Samia Suluhu ambaye ni mgombea mwenza wa Dk. John Pombe Magufuli amefanikiwa kuvunja ngome za wapinzani katika mikutano yake ya kampeni mjini Tanga baada ya wagombea udiwani watano wa ACT Wazalendo kujiunga na CCM pamoja na wanachama wengine 235 toka Tanga mjini kujiunga na CCM kwenye mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Usagara mkoani Tanga.
Akihutubia katika mkutano huo wa kampeni kunadi ilani ya CCM Tanga mjini uwanja wa Usagara, Bi. Samia Suluhu amewapokea wagombea udiwani watano kutoka ACT Wazalendo, wakiwemo Wilson Elia (wa Kata ya Duga), Gasper Maboko (Kata ya Nguvumali), Charles Luanda (Maweni) na Marry Scoty (Kata ya Tanga Sisi) pamoja na Sada Mbwambo (viti maalum).
Mbali na madiwani hao kukihama chama cha ACT, wanachama 235 kutoka ACT, CUF na Chadema wamejiunga na CCM kwenye mkutano huo wa Tanga mjini huku wengine 37 wakijiunga na CCM katika mkutano mwingine ulofanyika Jimbo la Muheza hivyo kutimiza wanachama 272 wapya kujiunga katika mikutano ya siku hiyo.
Akizungumza na wanaCCM na wananchi waliojitokeza mkutano wa Tanga Mjini, Bi. Suluhu amewaomba kuichagua CCM kurudi madarakani ili kuendeleza maendeleo iliyofikia katika maeneo mbalimbali, ikiwemo huduma za kijamii na miundombinu hasa ya barabara.
Bi. Samia amefanya mikutano minne mikubwa katika majimbo ya Mkinga, Pangani, Mheza na Tanga Mjini na mikutano midogo midongo sita alioifanya njiani akisimamishwa na wananchi wakitaka kumsikia alipokuwa akipita.
via Ippmedia --Edited by Denice Kazenzele
********************************************************************
MWANZA                            

Msajili wa vyama vya siasa nchini Mh.Jaji Francis Mutungi amewataka viongozi wa mathehebu ya dini,wamiliki wa vyombo vya habari na asasi za kiraia wasikubali kutumiwa na wanasiasa kuvuruga amani iliyodumu miaka 54 ya uhuru wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu 2015.
Wito huo umetolewa jijini Mwanza katika maadhimisho ya siku ya amani duniani ambapo kitaifa yamefanyika jijini humo na kuwahusisha, viongozi wa madhehebu ya dini, asasi za kiiraia, wasomi, walemavu, wamiliki wa vyombo vya habari na wandishi wa habari Mh.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la umoja wa mataifa linalojihusisha na utoaji elimu, sayansi na utamaduni kwa jamii UNESCO hapa nchini Bi.Zurmila Rodriguez amewataka watanzania kudumisha amani iliyopo miaka 54 ya uhuru hasa kwa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu 2015 kwa kumuenzi baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere ambaye alipigania ukombzi wa nchi za Afrika na kuitangaza Tanzania kuwa kisiwa cha amani duniani.
Kwa upande wake kaimu mkuu wa mkoa wa Mwanza mchungaji Baraka Konisaga amesikitishwa na vurugu za wananchi kuchukua sheria mikononi kwa kuvunja gari la jeshi la polisi vioo ambapo naibu kamishina wa polisi ambaye ni kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Charles Mkubo ameuhakikishia umoja wa mataifa kuwa jeshi la polisi Tanzania limejipanga kikamilifu kuimalisha ulinzi wakati wa kampeni, siku ya kupiga kura na siku ya kutangaza matokeo.
Edited by Denice Kazenzele
 *******************************************************************
DAR ES SALAAM         
Wadau wa uzalishaji dawa ukanda wa Afrika Mashariki wanakutana jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza kujadili muongozo wa utumiaji wa dawa unaozingatia viwango vya kimataifa ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya mkutano wa kisekta uliokutanisha mawaziri wa masuala ya afya wa ukanda huo.

Ajenda kuu ya mkutano huo ni namna nchi zote tano za Afrika Mashariki zinavyoweza kuwa na matumizi sawa na viwango vinavyofanana vya dawa pamoja na kuhamasisha uwekezaji zaidi kwenye uzalishaji wa dawa.

Asilimia 80 ya dawa zinazotumika nchini huagizwa kutoka nje ya nchi, tena zikiwa na viwango tofauti, nyingine zikiwa chini ya viwango na nyingine zinazokubalika kwa kiwango cha kimataifa, kutokana na nchi zinapozalishwa dawa hizo na namna zinavyoingizwa.

Pamoja na tofauti za viwango, mkutano huo umejadili matumizi sahihi ya dawa ambayo yamekuwa na athari kubwa kwa watumiaji hususan kusababisha usugu wa dawa.

Miongoni mwa wadau wakuu kwenye eneo hilo, ni Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini (TFDA) ambayo imezungumzia mfumo huo mpya wa wazalishaji wa dawa unaoanza kutekelezwa kikanda na Jumuiya ya Afrika Mashariki na kudai utakuwa na tija kwa watumiaji na kuondoa usugu ambao ulijitokeza wakati wa matumizi ya dawa ambazo azina viwango.

Edited by Denice Kazenzele
 *****************************************************************
PWANI                               
Imeelezwa kuwa lishe bora ni muhimu kwa ustawi wa watoto kiafya na kielimu hivyo ni vyema kwa serikali kuingiza katika katiba ya nchi inayotambua moja kwa moja haki za watoto.
Kauli hiyo imetolewa na mgombea udiwani kata ya kisarawe kwa tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA katika mdahalo uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe na kuwahusisha wagombea wa ngazi hiyo katika kata hiyo ili kuzungumzia ajenda za watoto kuzungumzwa katika jamii.
Akiinadi Ilani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo, Baraka Musa anayegombea udiwani kata ya Kisarawe, amesema chama chake kinaamini kuwa lishe bora ni muhimu kwa ustawi wa watoto kiafya na kielimu na endapo kitaingia madarakani kitahakikisha kinawekeza kwenye kupata Katiba inayotambua na kuzitaja moja kwa moja haki za watoto.
Naye mgombea wa udiwani wa kata hiyo kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Abel Mudo amesema endapo chama chake kitapata ridhaa ya kuendelea kuongoza nchi kitawekeza zaidi katika shule na kuhakikisha zina walimu wa kutosha na kwamba serikali yake imetengeneza mazingira rafiki na kutoa zana kwa watoto wenye ulemavu.
Mgombea huyo ameahidi kufanya kazi pamoja na wadau mbalimbali ili kuhakikisha wanapunguza ukatili kwa watoto na kukabiliana na matatizo  ya mimba za utotoni sambamba na kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa hadi kidato cha nne.
Edited by Denice Kazenzele
**************************************
KIMATAIFA:
OUAGADOUGOU                      

Jenerali Gilbert Diendere aliyefanya mapinduzi nchini Burkina Faso amesema yupo tayari kukabidhi serikali kwa utawala wa kiraia kama ilivyopendekezwa na wapatanishi.
Diendere ambaye alipindua serikali hiyo siku ya alhamisi wiki iliyopita amesema kuwa alifikia uamuzi huo kwa lengo la kile anachokiita kuepusha umwagaji mkubwa wa damu.
Burkina Demos

Kauli yake kukiri kukabidhi madaraka inakuja huku majeshi ya serikali yaki ukaribia mji mkuu wa Ouagadougou

Jeshi la Burkina Faso limeahidi kuwepo kwa hali ya Usalama kutokana na mapinduzi hayo,japo kuwa wameahidi kuto waangamiza waliofanya mapinduzi hayo iwapo tu watasalimisha silaha zao.

Hata hivyo kwa sasa Jeneral Diendere anadaiwa kujificha nyumbani kwa kiongozi wa kijadi Mogho Naaba.
bbcswahili/Re-Edited by Denice Kazenzele
 **************************************************************
 WASHINGTON                   
 
Scott Walker, ambaye ni miongoni mwa wagombea waliokuwa wakiwania kuteuliwa kugombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Republican amejiondoa katika kinyang'anyiro hicho.
Bwana Walker ambaye alikuwa gavana wa jimbo la Winscosin amesema amejitoa kwenye kampeni hizo ili kutoa nafasi kwa uteuzi wa mgombea muafaka atakayekabiliana na Donald Trump.
Mgombea huyo, ambaye alikuwa akiungwa mkono kwa wingi na wafuasi wa mrengo wa kulia, lakini hata hivyo katika kura ya maoni kiwango chake kilishuka baada ya kufanya vibaya katika midahalo.
Bbcswahili/Re-Edited by Denice Kazenzele
  ************************************************************
 MOGHADISHU                        SAA 06:00 MCHANA                         22.09.2015
picha hii haina uhusiano wa moja kwa moja na habari husika



Shambulizi lililotokea jana dhidi ya Ikulu ya Somalia mjini Mogadishu limesababisha vifo vya watu zaidi 9 na wengine 14 kujeruhiwa. 

Mabomu yaliyotegwa ndani ya gari yalilipuka usiku wa siku hiyo nje ya lango la Ikulu ya Somalia, na watu 9 wakiwemo askari wawili wa jeshi la serikali na wageni 3 waliuawa kwenye shambulizi hilo.
Siku hiyo maofisa wa serikali ya Somalia na baadhi ya wajumbe wa nchi nyingine walikuwa wakikutana kwenye Ikulu hiyo kujadili uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.
Wakati mlipuko huo unapotokea, washiriki wengi wa mkutano huo walikuwa wameondoka, lakini walikuwepo maofisa wachache waliobaki ambao ni kati ya waliouawa na kujeruhiwa.
Kundi la Al-Shabaab limetangaza kufanya shambulizi hilo dhidi ya maofisa wa serikali ya Somalia. 

Cri/Re-Edited by Denice Kazenzele

NAFASI 368 ZA KAZI ZIMEPIGANIWA NA WAOMBAJI MIL.2.3 NCHINI INDIA....

>>ni nafasi za ulinzi na uhudumu wa chai maofisini

>>maafisa wa serikaliwasema iwapo watafanyiwa intervie mmoja mmoja, itamalizika mwaka 2020,

>>wao wakili maisha nchini india ni magumu kutokana na uhaba wa ajira


Wakati nchi ya india ikitajwa kuwa ifikapo mwaka 2030 itaongoza kuwa na idadi kubwa ya watu baada ya takwimu za hivi sasa kuonesha kuwa nchi ya China ndio inayoshika nafasi ya kwanza kwa kuwa na Idadi kubwa ya watu Duniani ikiwa na jumla ya watu Bilioni 1.38, nafasi ya pili ni India ambayo ina jumla ya watu Bilioni 1.31, kati ya idadi ya Dunia nzima ya watu Bilioni 7 !!

TOP TEN YA VIMWANA WA NYOTA WA SOKA EPL 2015 HII HAPA


Tumezoea kuona mastaa kadhaa wa soka kuingia katika headlines na wapenzi wao, wakiwa wametoka out katika sehemu mbalimbali za starehe baada ya kazi nzuri walioifanya uwanjani. Stori kutoka talksport.com waliwahi kutoa May 2015 list ya Top 10 ya warembo wa mastaa wa soka wa Ligi Kuu Uingereza.
10- Edurne Garcia huyu ni mpenzi wa golikipa wa klabu ya Manchester United David de Gea.

Rais Kikwete Apewa Tuzo ya Utawala Bora Marekani

unnamed 

Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mheshimiwa Wilson Masilingi akimkabidhi Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Tuzo ya Utawala Bora ya Baraza la Biashara la Wana-Afrika Mashariki Waishio Marekani na nchi nyingine (East African Diaspora Business Council Award), Jumatatu, Septemba 21, 2015 mjini Washington, D.C. Balozi Masilingi ndiye alimwakilisha Dkt. Kikwete katika sherehe ya kukabidhi tuzo hiyo usiku wa jana, Jumapili, Septemba 20 kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, Dallas, Jimbo la Texas.

HAYA HAPA MAGAZETI YA TANZANIA LEO JUMANNE,SEPT 22,2015


UNAYAJUA MAZIWA YANAYOTAJWA KUWA NA MUONEKANO WA MOYO AU KOPA? TAZAMA HAPA LIST YA MAZIWA 10 DUNIANI YA MOYO.



Mtu wangu wa nguvu bado Malunde1 blog inakusogezea uzuri wa dunia, huenda umewahi kutembelea vivutio vingi vya utalii duniani lakini huenda hukuwahi kubahatika kufika wala kusikia kuhusu maziwa haya mazuri ya kuvutia yenye muonekano wa umbo la moyo au kopa. Hii ni stori ambayo nimekutana nayo mtandaoni mtu wangu wa nguvu, hivyo nikaona sio vibaya September 22 nikakusogezea karibu yako Top 10 ya maziwa yenye muonekano wa moyo duniani. Chanzo cha hii stori ni World – World Top Top. Huu ni muonekano wake kwa juu

1- Ziwa Shimshal – Pakistan

Hili ni ziwa lenye umbo la moyo na lipo katika bonde la Hunza Pakistan

Sunday, September 20

HATA KATIKA MECHI NA SIMBA NITAFUNGA TU

 
Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma amesema mechi dhidi ya Simba, itakuwa kama mechi nyingine na ana uhakikaa atafunga.

JESHI LA POLISI MKOANI DODOMA LIPO VIZURI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU MWEZI UJAO

JESHI la Polisi Mkoani hapa limesema katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wananchi wanapaswa kutii sheria, kanuni na taratibu za kampeni za uchaguzi bila kusubili shuruti.
 
Pia limesema limejipanga vizuri hivyo wananchi wasithubutu kufanya vurugu kwani hatua kali zitachukuliwa dhidi yao na kwamba wamejipanga vyema huku wakiwa na vifaa vya kutosha vya mawasiliano kama camera na vinasa sauti.

Saturday, September 19

MPYA KUMHUSU LUKE SHAW

2C78A77900000578-0-image-a-2_1442589564680

Mchezaji wa Machester united Luke Shaw alipata injury kwenye mechi UEFA dhidi ya PSV na kukimbizwa hospitali ya karibu na uwanja uliokua unafanyika mechi ile. Baada ya kupata matibabu kwenye hospital ya St Anna huko Eindhoven, Luke Shaw anategemea kurudi Manchester kwa ajili ya kuendelea na matibabu zaidi.

HAYA HAPA MATOKEO YA EPL LEO MECHI ZA JIONI, ARSENAL ACHEZEA VIWILI KWA MTUNGI



Gabriel is blocked by Chelsea players as he tries to  confront Diego Costa


Premier League
 
Chelsea 2 - 0 Arsenal

TAMBWE AIBUKA SHUJAA YANGA IKIWATUNGUA JKT RUVU 4-1


Mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe akishangilia moja ya goli lake alilofunga kwenye mchezo dhidi ya JKT Ruvu
Mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe akishangilia moja ya goli lake alilofunga kwenye mchezo dhidi ya JKT Ruvu
Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara timu ya Yanga, imeendelea kufanya kweli kwenye uwanja wa Taifa baada ya jioni ya leo kuibugiza JKT Ruvu jumla ya goli 4-1 kwenye mchezo wa raundi ya tatu ya ligi hiyo iliyoendelea leo.

Goli la kwanza la Yanga lilifungwa na mshambuliaji Donald Ngoma katiaka kipindi cha kwanza dakika ya 33 huku goli hilo lililodumu mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.
Yanga vs JKT Ruvu 
Kipindi cha pili Yanga walirudi wakiwa wamecharuka kwani dakika ya 48 kipindi cha pili Amis Tambwe aliifungia Yanga bao la pili,  dakikambili baadae Naftali Nashon akaifungia JKT Ruvu goli ambalo liliipa nguvu timu hiyo na kuanza kutafuta goli la kusawazisha.
Wakati JKT Ruvu wakiwa kwenye harakati za kutafuta goli la pili la kusawazisha, Amis Tambwe akapachika goli la tatu dakika ya 60 kwa upande wa Yanga ambalo ni goli lake la pili kwenye mechi ya leo huku Thabani Kamusoko akihitimisha kalamu ya magoli kwa upande wa Yanga kwa kufunga goli la nne dakika ya 87 ya mchezo.

HILI NDIO KUBWA KWA LEO KUTOKA KWA DK MAGUFULI WILAYANI CHATO

Dk Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa mwalimu wake wa darasa la kwanza marehemu, Cornel Pastory


Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akijinadi kwa wananchi huku akishangiliwa aliposimama kusalimia katika Mji wa Nyakanazi, wilayani Biharamulo, Mkoa wa Kagera leo.

MANENO ALIYOYAANDIKA ANNIE MKE WA 2 FACE KWENYE CAKE KATIKA BIRTHDAY YA MUMEWE NDIYO YALIYOKUWA KIVUTIO KIKUBWA.........



Huenda katika Sherehe ambazo staa wa Nigeria 2 Face Idibia amewahi kuzifanya hii ambayo ilifanyika jana September 18 2015 ilikuwa imekaa poa zaidi !!

JUMAMOSI YAKO ITAKUWA NJEMA KINOMA NOMA KAM UTAANZA NA VITUKO HIVI VYA KUKUTOA MBAVU AHAHAHAHAHAHA MI NIMEANZA!!!!








HAYA HAPA NDIO MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI SEPT 19,2015

 



Friday, September 18

MWAMERIKA ALIYEENDA KUTOA MSAADA KWA WAHANGA WA TETEMEKO ASIKITISHA WATU KWA KILICHOMKUTA!! FUATILIA KISA KIZIMA HAPA {VIDEO}

Dahlia Yehia alikuwa ni msichana mwenye furaha, amani na moyo wa kuwasaidia watu wenye shida lakini ndoto zake zilifupishwa baada ya safari yake ya kwenda Nepal kwenda vibaya!

NIMEONA NIKULETEE MIJENGO YA HOTEL ZA AJABU ZINAZOPATIKANA HUMU DUNIANI........


Teknolojia ya sasa inazidi kukua siku hadi siku, wataalamu wamekuwa wakibuni vitu mbalimbali duniani kwa lengo la kuleta ushindani.

WIZARA YA AFYA YAMTAKA MKEMIA MKUU ATAFUATILIA MATUMIZI YA SIGARA YA KIKO YA MAJI (SHISHA)

index 
 
………………………………….
WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii imeiagiza Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kufuatilia matumizi ya sigara ya kiko ya maji (Shisha) katika kumbi za starehe  za hapa nchini kwa kuwa sigara hizo zinahusishwa na  matumizi ya madawa ya kulevya.

USHAWAHI KUSIKIA NDOA YA FASTA FASTA? SASA HII IMEFUNGIWA BEACH MBELE YA WATU NANE......SOMA NA TAZAMA PICHA HAPA


Ronke na Lawson wamependana? Love yao hawakutaka masuala ya kusumbuana na ndugu masuala ya michango, vikao vya Harusi, kujaza watu Ukumbini.. wao kila kitu kimefanywa simple tu yani.

SERIKALI YAUJIBU UKAWA KUHUSU SAFARI YA RAIS NA GHARAMA,YADAI KUTOTUMIA HATA NUSU YA KIWANGO WALICHOKITAJA WAPINZANI

TAARIFA KWA UMMA - ZIARA ZA RAIS NJE

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 

Safari za Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete Nje ya Nchi.
 

Wizara imesikitishwa na taarifa za uongo zilitolewa katika vyombo vya habari kuwa Mhe. Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uongozi wake wa miaka 10 ametumia Shilingi trilioni 4 kwa ajili ya safari za kikazi nje ya nchi, ambazo ni wastani wa bajeti nzima ya wizara kwa miaka mitano (5).

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kutoa ufafanuzi kuwa tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aingie madarakani mwaka 2005, kiasi kikubwa kabisa cha bajeti kuwahi kutengwa kwa ajili ya safari za Viongozi Wakuu yaani Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu ni shilingi bilioni 50 ambazo zilitengwa kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015 kwa ajili ya Idara ya Itifaki. 


Kwa miaka mingine yote wastani umekuwa ni kati ya shilingi bilioni tano hadi 25 kulingana na mahitaji ya idara hiyo.
 

Ifahamike kuwa kiasi hicho cha shilingi bilioni 50 ni bajeti nzima ya Idara ya Itifaki, ambapo kuna fungu maalum kwa ajili ya ziara za viongozi. Fungu hilo linagharamia makundi makuu matano kama ifuatavyo:
 

1. Kundi la Rais wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;
 

2. Kundi la Makamu wa Rais wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;
 

3. Kundi la Waziri Mkuu wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;
 

4. Kundi la Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka nje ya nchi wanapotembelea Tanzania; na
 

5. Kundi la Wajumbe Maalum wanaokuja nchini kuleta taarifa muhimu kwa Rais.
 

Makundi yote haya hugaramiwa na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ndani ya bajeti ya Idara ya Itifaki kifungu cha Ziara za Viongozi.

Aidha uandaaji wa bajeti ya Wizara chini ya Idara ya Sera na Mipango unahusisha wadau wengine nje ya Wizara kama vile Kamati ya Bunge ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na hupitishwa kila mwaka na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tunapenda kuwaatahadharisha wananchi juu ya watu wanaotoa taarifa za uongo kwa madhumuni ya kujenga chuki dhidi ya Serikali. Ikumbukwe kuwa ziara za viongozi zinazoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje zina mafanikio makubwa kwa nchi na Watanzania kwa ujumla.

Wizara inaandaa taarifa ya ndefu ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara, changamoto na mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka kumi ya uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambayo itatolewa kwa umma kwa lengo la kutoa elimu zaidi.
 

                                                                                        Imetolewa na:
                                                    Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
                                             Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
                                                                                  17 Septemba 2015

Queen Darleen: Muziki Umenikosanisha Na Boyfriends Zangu

Queen Darleen ambaye pia ni dada yake na Diamond amesema ameachana na wanaume wengi kutokana familia za wanaume kutomkubali kwa kudai ni mhuni.
11264967_899675290067888_1156573801_n 
Darleen alisema ndugu wa upande wa wanaume wamekuwa wakichochotea maneno kwa watoto wao hali iliyosabisha kuachana.

Saturday, August 8