Thursday, September 24
Wednesday, September 23
HABARI KUTOKA RASI FM RADIO..SEPT 23 MCHANA
| picha na Maabara |
Waumini wa dini ya kiislamu duniani kote wanatarajia kusherehekea sikukuu ya Eid El Hajj hapo kesho ambapo kwa mkoa wa Dodoma ibada ya pamoja ya sikukuu ya swala ya eid el hajj I itakuwa katika uwanja wa jamhuri.
RAIS WA LA LIGA ATHIBITISHA KUWA FC BARCELONA MASHAKANI LA LIGA MUDA WOWOTE ITAONDELEWA....UNDANI UKO HAPA
Rais wa Ligi Kuu Hispania (LALIGA) Javier Tebas na waziri wa michezo wa Hispania Miguel Cardenal wamethibitisha kama Catalonia ikijitenga na kutoka katika umoja wa Hispania klabu ya FC Barcelona ambayo inatokea Catalonia haitashiriki Ligi Kuu Hispania.
ULIYAPATA MATOKEO YA JANA SEPT 22 KATI YA SUNDERLAND DHIDI YA MANCHESTER UNITED? CHEKI HAPA NA HIGHLIGHTS ZOTE ZA MAGOLI
>>
Yapo pia matokeo ya mechi nyingine za Capital one
Klabu ya Manchester City usiku wa September 22 ilikaribishwa na klabu ya Sunderland katika uwanja wa Stadium of Light kucheza mchezo wa Kombe la Capital One, mechi imemalizika kwa klabu ya Manchester City kuibuka na ushindi wa goli 4-1.
Baada ya majibu ya TWAWEZA kuipa CCM ushindi wa 66 %, kwa ufupi sana Lowassa kajibu haya pia yupo zitto kabwe,January makamba lakini magufuli JP hajasema chochote
ALIKIBA AFUNGUKA JUU YA RAIS AJAYE ANAYEMKUBALI, MCHEKI HAPA RAIS WAKE YEYE 2015
Wakati tukishuhudia wasanii kama kalla jeremiah, jack line wolper,Roma mkatoliki na wengineo wakiwa na mwelekeo wa kumshabikia mgombea urais kupitia ukawa yaani Edward Lowassa, huku pia JB,Aunty Ezekiel, Ray, Bi mwenda na wengineo nao wakimuunga mkono mgombea urais kupitia CCM John Pombe Magufuli, sasa rasmi msanii Ali Kiba nae amejiunga rasmi na kina Ray kumpa nguvu magufuli.
Hizi ndizo kurasa za mbele na nyuma za magazeti 17 ya kitanzania ya leoseptember 23 2015 ..
September 23 2015 ninazo tayari stori kubwakubwa kwenye kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania >>> Udaku, Hardnews na Michezo.
Jumla ya Magazeti 17 ya Tanzania tayari yamenifikia leo, nimekusogezea uzipate kurasa zake za mbele na za nyuma zilizobeba stori kubwa kwa leo.
Tuesday, September 22
RASI FM HABARI SAA 7:00 USIKU SEPT 22
Chama cha Wazazi wa Watoto Wenye
Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, Akili na Viungo (Chawaumavita) kimewataka wakina
baba kuacha tabia ya uoga ya kukimbia majukumu pindi wanapopata watoto wenye
ulemavu.
TAARIFA YA HABARI RASI FM RADIO SEPTEMBER 22.2015
KITAIFA:,
TANGA
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu
Hassan amevuna wanachama 272 Mkoani Tanga kutoka vyama mbalimbali vya upinzani
baada ya wanachama wa vyama hivyo kujiunga rasmi na CCM.
Bi. Samia Suluhu ambaye ni mgombea
mwenza wa Dk. John Pombe Magufuli amefanikiwa kuvunja ngome za wapinzani katika
mikutano yake ya kampeni mjini Tanga baada ya wagombea udiwani watano wa ACT
Wazalendo kujiunga na CCM pamoja na wanachama wengine 235 toka Tanga mjini
kujiunga na CCM kwenye mkutano mkubwa wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa
Usagara mkoani Tanga.
Akihutubia katika mkutano huo wa
kampeni kunadi ilani ya CCM Tanga mjini uwanja wa Usagara, Bi. Samia Suluhu amewapokea
wagombea udiwani watano kutoka ACT Wazalendo, wakiwemo Wilson Elia (wa Kata ya
Duga), Gasper Maboko (Kata ya Nguvumali), Charles Luanda (Maweni) na Marry
Scoty (Kata ya Tanga Sisi) pamoja na Sada Mbwambo (viti maalum).
Mbali na madiwani hao kukihama chama
cha ACT, wanachama 235 kutoka ACT, CUF na Chadema wamejiunga na CCM kwenye
mkutano huo wa Tanga mjini huku wengine 37 wakijiunga na CCM katika mkutano
mwingine ulofanyika Jimbo la Muheza hivyo kutimiza wanachama 272 wapya kujiunga
katika mikutano ya siku hiyo.
Akizungumza na wanaCCM na wananchi
waliojitokeza mkutano wa Tanga Mjini, Bi. Suluhu amewaomba kuichagua CCM kurudi
madarakani ili kuendeleza maendeleo iliyofikia katika maeneo mbalimbali,
ikiwemo huduma za kijamii na miundombinu hasa ya barabara.
Bi. Samia amefanya mikutano minne
mikubwa katika majimbo ya Mkinga, Pangani, Mheza na Tanga Mjini na mikutano
midogo midongo sita alioifanya njiani akisimamishwa na wananchi wakitaka
kumsikia alipokuwa akipita.
via Ippmedia --Edited by Denice Kazenzele
********************************************************************
MWANZA
Msajili wa vyama vya siasa nchini
Mh.Jaji Francis Mutungi amewataka viongozi wa mathehebu ya dini,wamiliki wa
vyombo vya habari na asasi za kiraia wasikubali kutumiwa na wanasiasa kuvuruga
amani iliyodumu miaka 54 ya uhuru wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu 2015.
Wito huo umetolewa jijini Mwanza
katika maadhimisho ya siku ya amani duniani ambapo kitaifa yamefanyika jijini humo
na kuwahusisha, viongozi wa madhehebu ya dini, asasi za kiiraia, wasomi,
walemavu, wamiliki wa vyombo vya habari na wandishi wa habari Mh.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika la
umoja wa mataifa linalojihusisha na utoaji elimu, sayansi na utamaduni kwa
jamii UNESCO hapa nchini Bi.Zurmila Rodriguez amewataka watanzania kudumisha
amani iliyopo miaka 54 ya uhuru hasa kwa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu
2015 kwa kumuenzi baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere ambaye
alipigania ukombzi wa nchi za Afrika na kuitangaza Tanzania kuwa kisiwa cha
amani duniani.
Kwa upande wake kaimu mkuu wa mkoa
wa Mwanza mchungaji Baraka Konisaga amesikitishwa na vurugu za wananchi
kuchukua sheria mikononi kwa kuvunja gari la jeshi la polisi vioo ambapo naibu
kamishina wa polisi ambaye ni kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Charles Mkubo
ameuhakikishia umoja wa mataifa kuwa jeshi la polisi Tanzania limejipanga
kikamilifu kuimalisha ulinzi wakati wa kampeni, siku ya kupiga kura na siku ya
kutangaza matokeo.
Edited by Denice Kazenzele
*******************************************************************
DAR ES SALAAM
Ajenda kuu ya mkutano huo ni namna nchi zote tano za Afrika Mashariki zinavyoweza kuwa na matumizi sawa na viwango vinavyofanana vya dawa pamoja na kuhamasisha uwekezaji zaidi kwenye uzalishaji wa dawa.
Asilimia 80 ya dawa zinazotumika nchini huagizwa kutoka nje ya nchi, tena zikiwa na viwango tofauti, nyingine zikiwa chini ya viwango na nyingine zinazokubalika kwa kiwango cha kimataifa, kutokana na nchi zinapozalishwa dawa hizo na namna zinavyoingizwa.
Pamoja na tofauti za viwango, mkutano huo umejadili matumizi sahihi ya dawa ambayo yamekuwa na athari kubwa kwa watumiaji hususan kusababisha usugu wa dawa.
Miongoni mwa wadau wakuu kwenye eneo hilo, ni Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini (TFDA) ambayo imezungumzia mfumo huo mpya wa wazalishaji wa dawa unaoanza kutekelezwa kikanda na Jumuiya ya Afrika Mashariki na kudai utakuwa na tija kwa watumiaji na kuondoa usugu ambao ulijitokeza wakati wa matumizi ya dawa ambazo azina viwango.
Edited by Denice Kazenzele
*****************************************************************
PWANI
Imeelezwa
kuwa lishe bora ni muhimu kwa ustawi wa
watoto kiafya na kielimu hivyo ni vyema kwa serikali kuingiza katika katiba ya
nchi inayotambua moja kwa moja haki za watoto.
Kauli hiyo imetolewa na mgombea udiwani kata ya kisarawe kwa tiketi ya
chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA katika mdahalo uliofanyika katika
ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe na kuwahusisha wagombea wa ngazi
hiyo katika kata hiyo ili kuzungumzia ajenda za watoto kuzungumzwa katika jamii.
Akiinadi Ilani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo, Baraka Musa
anayegombea udiwani kata ya Kisarawe, amesema chama chake kinaamini kuwa lishe
bora ni muhimu kwa ustawi wa watoto kiafya na kielimu na endapo kitaingia
madarakani kitahakikisha kinawekeza kwenye kupata Katiba inayotambua na kuzitaja
moja kwa moja haki za watoto.
Naye mgombea wa udiwani wa kata hiyo kupitia tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi Abel Mudo amesema endapo chama chake kitapata ridhaa ya kuendelea
kuongoza nchi kitawekeza zaidi katika shule na kuhakikisha zina walimu wa
kutosha na kwamba serikali yake imetengeneza mazingira rafiki na kutoa zana kwa
watoto wenye ulemavu.
Mgombea huyo ameahidi kufanya kazi pamoja na wadau mbalimbali ili
kuhakikisha wanapunguza ukatili kwa watoto na kukabiliana na matatizo ya
mimba za utotoni sambamba na kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa hadi kidato cha
nne.
Edited by Denice Kazenzele
**************************************
KIMATAIFA:
OUAGADOUGOU
Jenerali Gilbert
Diendere aliyefanya mapinduzi nchini Burkina Faso amesema yupo tayari kukabidhi
serikali kwa utawala wa kiraia kama ilivyopendekezwa na wapatanishi.
Kauli yake kukiri kukabidhi madaraka inakuja huku majeshi ya serikali yaki ukaribia mji mkuu wa Ouagadougou
Jeshi la Burkina Faso limeahidi kuwepo kwa hali ya Usalama kutokana na mapinduzi hayo,japo kuwa wameahidi kuto waangamiza waliofanya mapinduzi hayo iwapo tu watasalimisha silaha zao.
Hata hivyo kwa sasa Jeneral Diendere anadaiwa kujificha nyumbani kwa kiongozi wa kijadi Mogho Naaba.
bbcswahili/Re-Edited by Denice Kazenzele
**************************************************************
WASHINGTON
Mgombea huyo, ambaye alikuwa akiungwa mkono kwa wingi na wafuasi wa mrengo wa kulia, lakini hata hivyo katika kura ya maoni kiwango chake kilishuka baada ya kufanya vibaya katika midahalo.
Bbcswahili/Re-Edited by Denice Kazenzele
************************************************************
MOGHADISHU SAA 06:00 MCHANA 22.09.2015
| picha hii haina uhusiano wa moja kwa moja na habari husika |
Shambulizi lililotokea jana dhidi ya Ikulu ya Somalia mjini Mogadishu limesababisha vifo vya watu zaidi 9 na wengine 14 kujeruhiwa.
Mabomu yaliyotegwa ndani ya gari yalilipuka usiku wa siku hiyo nje ya lango la Ikulu ya Somalia, na watu 9 wakiwemo askari wawili wa jeshi la serikali na wageni 3 waliuawa kwenye shambulizi hilo.
Siku hiyo maofisa wa serikali ya Somalia na baadhi ya wajumbe wa nchi nyingine walikuwa wakikutana kwenye Ikulu hiyo kujadili uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.
Wakati mlipuko huo unapotokea, washiriki wengi wa mkutano huo walikuwa wameondoka, lakini walikuwepo maofisa wachache waliobaki ambao ni kati ya waliouawa na kujeruhiwa.
Kundi la Al-Shabaab limetangaza kufanya shambulizi hilo dhidi ya maofisa wa serikali ya Somalia.
Cri/Re-Edited by Denice Kazenzele
NAFASI 368 ZA KAZI ZIMEPIGANIWA NA WAOMBAJI MIL.2.3 NCHINI INDIA....
>>ni nafasi za ulinzi na uhudumu wa chai maofisini
>>maafisa wa serikaliwasema iwapo watafanyiwa intervie mmoja mmoja, itamalizika mwaka 2020,
>>wao wakili maisha nchini india ni magumu kutokana na uhaba wa ajira
Wakati nchi ya india ikitajwa kuwa ifikapo mwaka 2030 itaongoza kuwa na idadi kubwa ya watu baada ya takwimu za hivi sasa kuonesha kuwa nchi ya China ndio inayoshika nafasi ya kwanza kwa kuwa na Idadi kubwa ya watu Duniani ikiwa na jumla ya watu Bilioni 1.38, nafasi ya pili ni India ambayo ina jumla ya watu Bilioni 1.31, kati ya idadi ya Dunia nzima ya watu Bilioni 7 !!
TOP TEN YA VIMWANA WA NYOTA WA SOKA EPL 2015 HII HAPA
Tumezoea kuona mastaa kadhaa wa soka
kuingia katika headlines na wapenzi wao, wakiwa wametoka out katika
sehemu mbalimbali za starehe baada ya kazi nzuri walioifanya uwanjani.
Stori kutoka talksport.com waliwahi kutoa May 2015 list ya Top 10 ya warembo wa mastaa wa soka wa Ligi Kuu Uingereza.
10- Edurne Garcia huyu ni mpenzi wa golikipa wa klabu ya Manchester United David de Gea.
Rais Kikwete Apewa Tuzo ya Utawala Bora Marekani
Balozi
wa Tanzania nchini Marekani, Mheshimiwa Wilson Masilingi akimkabidhi
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Tuzo ya Utawala Bora ya Baraza la
Biashara la Wana-Afrika Mashariki Waishio Marekani na nchi nyingine
(East African Diaspora Business Council Award), Jumatatu, Septemba 21,
2015 mjini Washington, D.C. Balozi Masilingi ndiye alimwakilisha Dkt.
Kikwete katika sherehe ya kukabidhi tuzo hiyo usiku wa jana, Jumapili,
Septemba 20 kwenye Hoteli ya Hyatt Regency, Dallas, Jimbo la Texas.
UNAYAJUA MAZIWA YANAYOTAJWA KUWA NA MUONEKANO WA MOYO AU KOPA? TAZAMA HAPA LIST YA MAZIWA 10 DUNIANI YA MOYO.
Mtu wangu wa nguvu bado Malunde1 blog
inakusogezea uzuri wa dunia, huenda umewahi kutembelea vivutio vingi vya
utalii duniani lakini huenda hukuwahi kubahatika kufika wala kusikia
kuhusu maziwa haya mazuri ya kuvutia yenye muonekano wa umbo la moyo au
kopa. Hii ni stori ambayo nimekutana nayo mtandaoni mtu wangu wa nguvu,
hivyo nikaona sio vibaya September 22 nikakusogezea karibu yako Top 10
ya maziwa yenye muonekano wa moyo duniani. Chanzo cha hii stori ni World – World Top Top. Huu ni muonekano wake kwa juu
1- Ziwa Shimshal – Pakistan
Hili ni ziwa lenye umbo la moyo na lipo katika bonde la Hunza Pakistan
Sunday, September 20
JESHI LA POLISI MKOANI DODOMA LIPO VIZURI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU MWEZI UJAO
JESHI la Polisi Mkoani hapa limesema katika kuelekea
kwenye uchaguzi mkuu wananchi wanapaswa kutii sheria, kanuni na taratibu za
kampeni za uchaguzi bila kusubili shuruti.
Pia limesema limejipanga vizuri hivyo wananchi
wasithubutu kufanya vurugu kwani hatua kali zitachukuliwa dhidi yao na kwamba
wamejipanga vyema huku wakiwa na vifaa vya kutosha vya mawasiliano kama camera
na vinasa sauti.
Saturday, September 19
MPYA KUMHUSU LUKE SHAW
Mchezaji wa Machester united Luke Shaw alipata injury kwenye mechi UEFA dhidi ya PSV na kukimbizwa hospitali ya karibu na uwanja uliokua unafanyika mechi ile. Baada ya kupata matibabu kwenye hospital ya St Anna huko Eindhoven, Luke Shaw anategemea kurudi Manchester kwa ajili ya kuendelea na matibabu zaidi.
TAMBWE AIBUKA SHUJAA YANGA IKIWATUNGUA JKT RUVU 4-1
Mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe akishangilia moja ya goli lake alilofunga kwenye mchezo dhidi ya JKT Ruvu
Mabingwa watetezi wa ligi kuu
Tanzania bara timu ya Yanga, imeendelea kufanya kweli kwenye uwanja wa
Taifa baada ya jioni ya leo kuibugiza JKT Ruvu jumla ya goli 4-1 kwenye
mchezo wa raundi ya tatu ya ligi hiyo iliyoendelea leo.
Goli la kwanza la Yanga
lilifungwa na mshambuliaji Donald Ngoma katiaka kipindi cha kwanza
dakika ya 33 huku goli hilo lililodumu mpaka kipindi cha kwanza
kinamalizika.
Kipindi
cha pili Yanga walirudi wakiwa wamecharuka kwani dakika ya 48 kipindi
cha pili Amis Tambwe aliifungia Yanga bao la pili, dakikambili baadae
Naftali Nashon akaifungia JKT Ruvu goli ambalo liliipa nguvu timu hiyo
na kuanza kutafuta goli la kusawazisha.
Wakati JKT Ruvu wakiwa kwenye
harakati za kutafuta goli la pili la kusawazisha, Amis Tambwe akapachika
goli la tatu dakika ya 60 kwa upande wa Yanga ambalo ni goli lake la
pili kwenye mechi ya leo huku Thabani Kamusoko akihitimisha kalamu ya
magoli kwa upande wa Yanga kwa kufunga goli la nne dakika ya 87 ya
mchezo.
HILI NDIO KUBWA KWA LEO KUTOKA KWA DK MAGUFULI WILAYANI CHATO
MANENO ALIYOYAANDIKA ANNIE MKE WA 2 FACE KWENYE CAKE KATIKA BIRTHDAY YA MUMEWE NDIYO YALIYOKUWA KIVUTIO KIKUBWA.........
Huenda katika Sherehe ambazo staa wa
Nigeria 2 Face Idibia amewahi kuzifanya hii ambayo ilifanyika jana
September 18 2015 ilikuwa imekaa poa zaidi !!
Friday, September 18
MWAMERIKA ALIYEENDA KUTOA MSAADA KWA WAHANGA WA TETEMEKO ASIKITISHA WATU KWA KILICHOMKUTA!! FUATILIA KISA KIZIMA HAPA {VIDEO}
Dahlia Yehia alikuwa
ni msichana mwenye furaha, amani na moyo wa kuwasaidia watu wenye shida
lakini ndoto zake zilifupishwa baada ya safari yake ya kwenda Nepal kwenda vibaya!
NIMEONA NIKULETEE MIJENGO YA HOTEL ZA AJABU ZINAZOPATIKANA HUMU DUNIANI........
WIZARA YA AFYA YAMTAKA MKEMIA MKUU ATAFUATILIA MATUMIZI YA SIGARA YA KIKO YA MAJI (SHISHA)
USHAWAHI KUSIKIA NDOA YA FASTA FASTA? SASA HII IMEFUNGIWA BEACH MBELE YA WATU NANE......SOMA NA TAZAMA PICHA HAPA
Ronke na Lawson wamependana?
Love yao hawakutaka masuala ya kusumbuana na ndugu masuala ya michango,
vikao vya Harusi, kujaza watu Ukumbini.. wao kila kitu kimefanywa
simple tu yani.
SERIKALI YAUJIBU UKAWA KUHUSU SAFARI YA RAIS NA GHARAMA,YADAI KUTOTUMIA HATA NUSU YA KIWANGO WALICHOKITAJA WAPINZANI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Safari za Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete Nje ya Nchi.
Wizara imesikitishwa na taarifa za uongo zilitolewa katika vyombo vya habari kuwa Mhe. Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uongozi wake wa miaka 10 ametumia Shilingi trilioni 4 kwa ajili ya safari za kikazi nje ya nchi, ambazo ni wastani wa bajeti nzima ya wizara kwa miaka mitano (5).
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inapenda kutoa ufafanuzi kuwa tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aingie madarakani mwaka 2005, kiasi kikubwa kabisa cha bajeti kuwahi kutengwa kwa ajili ya safari za Viongozi Wakuu yaani Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu ni shilingi bilioni 50 ambazo zilitengwa kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015 kwa ajili ya Idara ya Itifaki.
Kwa miaka mingine yote wastani umekuwa ni kati ya shilingi bilioni tano hadi 25 kulingana na mahitaji ya idara hiyo.
Ifahamike kuwa kiasi hicho cha shilingi bilioni 50 ni bajeti nzima ya Idara ya Itifaki, ambapo kuna fungu maalum kwa ajili ya ziara za viongozi. Fungu hilo linagharamia makundi makuu matano kama ifuatavyo:
1. Kundi la Rais wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;
2. Kundi la Makamu wa Rais wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;
3. Kundi la Waziri Mkuu wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;
4. Kundi la Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka nje ya nchi wanapotembelea Tanzania; na
5. Kundi la Wajumbe Maalum wanaokuja nchini kuleta taarifa muhimu kwa Rais.
Makundi yote haya hugaramiwa na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ndani ya bajeti ya Idara ya Itifaki kifungu cha Ziara za Viongozi.
Aidha uandaaji wa bajeti ya Wizara chini ya Idara ya Sera na Mipango unahusisha wadau wengine nje ya Wizara kama vile Kamati ya Bunge ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na hupitishwa kila mwaka na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tunapenda kuwaatahadharisha wananchi juu ya watu wanaotoa taarifa za uongo kwa madhumuni ya kujenga chuki dhidi ya Serikali. Ikumbukwe kuwa ziara za viongozi zinazoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje zina mafanikio makubwa kwa nchi na Watanzania kwa ujumla.
Wizara inaandaa taarifa ya ndefu ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara, changamoto na mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka kumi ya uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambayo itatolewa kwa umma kwa lengo la kutoa elimu zaidi.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
17 Septemba 2015
Queen Darleen: Muziki Umenikosanisha Na Boyfriends Zangu
Monday, August 17
Saturday, August 8
IJUE HISTORIA YA MECHI ZA UFUNGUZI WA LIGI KUU ENGLAND
Wednesday, July 29
WATOTO ZAIDI YA LAKI NANE WA WAWA WAKIMBIZI KUTOKANA NA BOKO HARAM
Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa(Unicef) umeeleza wasiwasi wake kuhusu kuendelea hujuma za kundi la Boko Haram zilizosababisha mamia ya maelfu ya watoto nchini Nigeria kuwa wakimbizi.
Subscribe to:
Posts (Atom)





