Wednesday, November 18

KOCHA WA YANGA..PLUIJM ALIA CHALENJI KUHARIBU PROGRAMU NA KAMBI NZIMA.....


Yanga imeshindwa kuingia kambini kujiandaa na Ligi Kuu Bara kutokana na michuano ya Kombe la Chalenji iliyopangwa kuanza Novemba 20 jijini Addis Ababa, Ethiopia.


Yanga hivi sasa inaendelea na maandalizi ya ligi kuu chini ya Kocha Mkuu, Mholanzi, Hans van Der Pluijm na Juma Mwambusi wakati ligi hiyo ikisimama.

Pluijm amesema ni ngumu kuifuata programu aliyoipanga wakati ligi kuu ikisimama kutokana na nusu ya wachezaji kuwepo vikosi vya timu zao za taifa.

Pluijm alisema, katika ripoti yake aliomba mechi tano za kirafiki za kimataifa pamoja na kambi ya pamoja ya kujiandaa na ligi hiyo katika kuhakikisha wanautetea ubingwa wao.

“Timu inaendelea na mazoezi yake ya pamoja ikiwa na mchanganyiko wa wachezaji wa U20 baada ya nusu ya wachezaji wa timu kubwa kuwepo kwenye timu zao za taifa.

“Hivyo hivi sasa siwezi nikafanya chochote ikiwemo kucheza mechi za kirafiki za kimataifa, pamoja na kambi ya kujiandaa na ligi kuu iliyosimama hadi pale wachezaji wote watakaporejea kujiunga na wenzao,” alisema Pluijm.

ETI LAZIMA WAONDOKE...BOMOA BOMOA MWENGE JIJINI DAR ES SALAAM LEO.......

Tingatinga likiendelea na kazi ya kubomoa nyumba na vibanda vya biashara vilivyojengwa isivyo halali katika maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam leo huku baadhi ya wananchi wakijaribu kunusuru baadhi ya mali.
Wananchi wakijaribu kuokoa mali zao baada ya maduka na nyumba kadhaa zilizojengwa isivyohalali kuvunjwa katika maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam

Polisi Marekani yawatia nguvuni wanaharakati weusi...


Polisi Marekani yawatia nguvuni wanaharakati weusi
Maafisa wa polisi nchini Marekani wamewatia mbaroni zaidi ya wanaharakati 50 waliokuwa wakishiriki maadamano katika jimbo la Minnesota. Mamia ya wanaharakati hao wamefanya maandamano ya kukashifu dhulma wanazopitia watu weusi nchini humo.
Chini ya kaulimbiu “Black Lives Matter” waandamanaji hao walifunga barabara kuu ya Minnesota huku wakiwa wamebeba mabango na maberamu yaliyokuwa na jumbe za kulaani ubaguzi wa rangi. 
Maandamano hayo yalinuia kuishinikiza polisi ya Minnesota kufafanua sababu za kuuawa kijana wa miaka 24 kwa jina Jamar Clack, mikononi mwa polisi katika jimbo hilo Jumapili iliyopita.

Wanachama wa Boko Haram mikononi mwa Cameroon..... Cameroon yawakamata wanachama wa Boko Haram

Jeshi la Cameroon limetangaza kuwa limewatia nguvuni wanachama kadhaa wa kundi la kigaidi la Boko Haram.
Cameroon yawakamata wanachama wa Boko HaramJeshi hilo limesema wanachama hao 19 wa kundi la Boko Haram wametiwa nguvuni katika kitongoji cha Ketta karibu na mpaka wa nchi hiyo na Nigeria katika operesheni iliyofanywa na jeshi la anga na la nchi kavu la nchi hiyo.
Vyombo vya jeshi la Cameroon vimesema kuwa idadi nyingine ya wapiganaji wa kundi la kigaidi la Boko Haram imeangamizwa katika mashambulizi yaliyoendelea kwa kipindi cha masaa mawili.
Jeshi la Cameroon lilianzisha operesheni kali ya kuwasaka na kuwaangamiza wanachama wa kundi la kiwahabi na kigaidi la Boko Haram baada ya wanachama wake kuvamia eneo la kaskazini mwa nchi hiyo na kuua idadi kubwa ya raia wa eneo hilo.  

JESHI IMARA...CAR yataka isaidiwe kuimarisha jeshi lake....


CAR yataka isaidiwe kuimarisha jeshi lake
Mkuu wa Baraza la Mpito la Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ferdinand Alexandre Nguendet ameitaka jamii ya kimataifa kuisaidia nchi yake kuimarisha uwezo wa jeshi ili kukabiliana na hali mbaya ya kiusalama katika nchi hiyo. 
Nguendet amefafanua kuwa, serikali ina mpango wa kuwachukua vijana 1000 kutoka kila jimbo na kuwapa mafunzo ya kijeshi na kwa njia hiyo taifa litaweza kupata jeshi jipya na imara. 
 Jamhuri ya Afrika ya Kati ina majimbo 77 na endapo mpango huo wa serikali utatekelezwa, jeshi jipya la nchi hiyo litakuwa na wanajeshi elfu 77. 
 Ferdinand Alexandre Nguendet amesema njia pekee ya kurejesha amani na utulivu Jamhuri ya Afrika ya Kati ni kuwa na jeshi imara na lenye uwezo wa kulinda mipaka ya nchi lakini pia kudhibiti hali ya mambo ndani ya nchi.

Rais wa Rwanda..jana..Baraza la Seneti Rwanda lapitisha mabadiliko ya muhula wa urais....

Bunge la Rwanda

Bunge la Rwanda


Baraza la seneti nchini Rwanda limepitisha mabadiliko mapya ya kipengele cha katiba kitakachomruhusu Rais Paul kagame kuendelea kubaki madarakani hadi mwaka 2034.
Uwamuzi huo ulichukuliwa kwa sauti moja siku ya Alhamis. Mabadiliko yaliyopendekezwa yatafikishwa mbele ya wananchi ili kuweza kupiga  kura ya maoni ambayo inatarajiwa kupata ushindi kiurahisi. 
Rais wa Rwanda, Paul Kagame.
Rais wa Rwanda, Paul Kagame.
 
Rais Kagame mwenye umri wa miaka 58, ameiongoza nchi ya Rwanda tangu jeshi lake lilipomaliza mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 na kuwaondoa madarakani wahutu wenye msimamo mkali nchini humo. Chini ya sheria iliyopo hivi sasa, bwana Kagame anatakiwa kujiuzulu mwishoni mwa muhula wake wa pili madarakani mwaka 2017.

URUSI: Marekani inafanya mchezo mchafu Syria....


Russia: Marekani inafanya mchezo mchafu Syria
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amesema Marekani inaendeleza mchezo mchafu na hatari nchini Syria, hatua inayofanya kuwa vigumu kubainisha nia ya Washington kuhusu mzozo wa nchi hiyo ya Kiarabu. Sergey Lavrov amesema Marekani ipo kwenye kinamasi kwa kutoa misimamo ya kukinzana kuhusu mgogoro wa Syria.
 Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia amesema kwa upande mmoja Marekani inaunga mkono kundi la kitakfiri la Daesh ili liangushe serikali halali ya Rais Bashar al-Assad, huku upande mwingine ikipinga mpango wa kundi hilo la kigaidi kutwaa madaraka iwapo litafanikiwa kuuangusha utawala wa Assad. Lavrov amekariri kuwa, mashambulizi ya anga ya jeshi la Marekani nchini Syria hayajazaa matunda kufikia sasa huku akipuuzilia mbali madai ya Washington kwamba vikosi vya Russia vinashambulia makazi ya raia nchini Syria.
 Hii ni katika hali ambayo, Uungaji mkono wa hali na mali wa Marekani na baadhi ya nchi za eneo ikiwemo Saudi Arabia, Qatar na Uturuki kwa wapinzani wa Syria tangu mwaka 2011 hadi sasa, umesababisha magaidi kutenda jinai za kutisha katika nchi za eneo hususan Syria na Iraq.


MAKUBALIANO...IAEA yapongeza makubaliano ya nyuklia ya Iran....


IAEA yapongeza makubaliano ya nyuklia ya Iran
Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA amepongeza kile alichokitaja kuwa ‘maendeleo mazuri’ kuhusu makubaliano ya nyuklia ya Iran katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. 
Akihutubia kongamano la 17 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapo jana mjini New York nchini Marekani, Yukiya Amano amesema makubaliano hayo yanadhihirisha kuwa masuala mazito ya kimataifa yanaweza kutatuliwa kwa njia za kidiplomasia. 
Amesema shirika hilo linajiandaa kuwasilisha ripoti ya mwisho ya uchunguzi wake kuhusu miradi ya nyukia ya Iran kufikia Disemba 15.
 Mkurugenzi Mkuu wa IAEA amepongeza juhudi za pande zote katika mazungumzo ya kufikiwa makubaliano ya nyuklia ya Iran, ikiwemo Tehran, kundi la 5+1 na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Itakumbukwa kuwa Iran na kundi la 5+1 zilifikia mapatano ya nyuklia huko Vienna, Austria mnamo Julai 14.


Marufuku Kuvaa....Senegal yapiga marufuku vazi la burqa.....

Senegal yapiga marufuku vazi la burqaSerikali ya Senegal imetoa taarifa rasmi ya kupiga marufuku vazi la stara la burqa, linalovaliwa na wanawake wa Kiislamu. Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo ya Kiafrika imesema kuwa, ni marufuku kuanzia sasa kuvaa burqa nchini humo, kutokana na sababu zilizotajwa kuwa za kiusalama. 
Gazeti la L’Observanteur la nchi hiyo limesema kuwa Rais Macky Sall ametia saini sheria hiyo, kufuatia mashinikizo kutoka kwa taasisi za kiusalama na kiulinzi za nchi hiyo.
 Hii ni katika hali ambayo, katika mkutano wa usalama na amani wa bara Afrika uliofanyika Jumatatu iliyopita mjini Dakar, Rais Sall alidokeza kuwa vazi hilo linafanya vita dhidi ya ugaidi kuwa vigumu. 
Miezi michache iliyopita, Cameroon nayo ilipiga marufuku vazi hilo la heshima la Kiislamu.
 Viongozi wa Cameroon walichukua uamuzi huo baada ya kujiri mlipuko uliouwa watu 13 na kujeruhi wengine 31 mwezi Julai mwaka huu.


UN: Watoto laki 5 wakabiliwa na utapia mlo Yemen.......

UN: Watoto laki 5 wakabiliwa na utapia mlo YemenMfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF umesema watoto zaidi ya laki 5 nchini Yemen wanakabiliwa na hatari ya kupoteza maisha kutokana na utapia mlo.
Mkuu wa mfuko huo Anthony Lake ameeleza hofu yake ya kuongezeka idadi hiyo na kwamba hatua za dharura zisipochukuliwa, huenda tatizo hilo likageuka na kuwa mzigo kwa jamii ya kimataifa.
 Hii ni kati hali ambayo, Saudi Arabia inaendelea kuua raia wasio na hatia nchini Yemen huku ikipuuza miito ya kusitisha hujuma zake za kinyama dhidi ya nchi hiyo masikini ya Kiarabu.
Hivi karibuni Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu lililaani kuendelea mashambulio ya Saudi Arabia dhidi ya hospitali na vituo vya afya huko Yemen. 
Saudi Arabia na waitifaki wake tarehe 26 Machi mwaka huu walianzisha mashambulizi dhidi ya wananchi wa Yemen kwa kisingizio cha kuirejesha madarakani serikali iliyojiuzulu.
 Raia zaidi ya 7,200 wameuawa na wengine wengi kulazimika kuwa wakimbizi kutokana na mashambulizi hayo huku miundo mbinu ya nchi hiyo ikiharibiwa vibaya.

Ugaidi: Wakimbizi Syria wabanwa.....


Kitengo cha misaada cha umoja wa mataifa kimetoa onyo juu ya suala la wakimbizi kutoka Syria kwamba hawapaswi kupewa uhuru mkubwa kufuatia shambulio la mjini Paris.
Baadhi ya taarifa zinasema kwamba mmoja wa washambuliaji wa Paris,aliingia Ulaya kama mkimbizi akitokea nchini Syria.
Wanasiasa kadhaa kutoka umoja wa Ulaya wametoa wito wa kusitishwa kwa zoezi la kuwapokea wahamiaji wanaofurika kuingia katika nchi za umoja wa Ulaya,ambao huvuka bahari ya Atlantic ingawa mpaka sasa majimbo takribani kumi na mawili ya Marekani wamesha sitisha zoezi la kupokea wahamiaji wanaotoka nchini Syria.
Umoja wa mataifa unaamini kwamba uchunguzi yakinifu wa wakimbizi wanapowasili katika maeneo wanayotafuta hifadhi,na haki ya kugawana mzigo wa huduma za wahamiaji na wakimbizi,kutasaidi kuwatambua ikiwa kuna shaka yoyote ya kiusalama pindi viashiria vitakapo ng'amuliwa.

Somalia yafungua tena ubalozi Marekani.....2015

Somalia itafungua tena ubalozi wake nchini Marekani leo miaka 25 baada ya ubalozi huo kufungwa.
Mwandishi wa BBC Abdullahi Abdi anasema hii ni hatua kubwa sana kwa Somalia na kwa Wasomali karibu 200,000 wanaoishi Marekani.
Maafisa wa serikali ya Somalia wanasema kufunguliwa kwa ni ishara ya hatua zilizopigwa tangu kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo 1991.
Uhusiano kati ya Somalia na Marekani umekuwa ukiimarika tangu Agosti 2012, Somalia ilipofikisha kikomo kipindi cha mpito na kuteua viongozi wapya.
Rais Obama aliteua balozi wa kwanza wa Marekani Somalia Februari mwaka huu, na miezi miwili baadaye waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani John Kerry akawa waziri wa kwanza wa kigeni wa Marekani kuzuru Mogadishu.
Somalia nayo iliteua balozi wa kuiwakilisha Marekani.
Licha ya hatua hiyo inayoashiria kuimarika kwa hali Somalia, hali ya usalama bado haijadhibitiwa na mashambulio ya mara kwa mara ya kundi la al-Shabab huripotiwa, hasa Mogadishu.

MAUAJI..Watu 32 wauawa kaskazini mwa Nigeria........


Watu 32 wameuawa kwenye shambulio la bomu la kujitoa mhanga katika mji wa Yola, kaskazini mashariki mwa Nigeria. Wengine 80 wamejeruhiwa.
Maafisa wa huduma za dharura wanasema miili ya waliofariki imepelekwa vyumba vya kuhifadhia maiti huku waliojeruhiwa wakipelekwa hospitalini.
Baadhi ya majeruhi walikuwa wamevunjika miguu na mikono.
Walioshuhudia shambulio hilo wanasema lilikuwa kubwa kiasi kwamba mlipuko ulisikika kote jijini.
Shambulio hilo lilitokea karibu na soko la mboga majira ya jioni.
Mji wa Yola umekuwa ukishambuliwa mara kwa mara, anasema mwandishi wa BBC aliye Abuja Abdullahi Kaura Abubakar.
Mji huo umeshuhudia milipuko miwili ya mabomu iliyoua watu zaidi ya hamsini mwaka huu na mojawapo wa miji iliyoathirika na mashambulio ya wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram.

Anayedaiwa kufuja fedha za Boko Haram kukamatwa.....


Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameagiza kukamatwa kwa afisa mmoja mkuu serikalini kwa tuhuma za kuiba zaidi ya dola bilioni 2 zilizotengewa vita dhidi ya kundi la Boko Haram.

Kanali Sambo Dasuki ambaye alikuwa mshauri wa kitaifa kuhusu maswala ya usalama kwa aliyekuwa rais Goodluck Jonathan ,ameshtakiwa kwa kutoa kandarasi bandia za kununua helikopta 12,ndege 4 za kijeshi na silaha.
Lakini vifaa hivyo havijawasili na mshauri huyo wa zamani anadaiwa kuiba fedha hizo.Tayari amekana madai hayo.
Msemaji wa rais Buhari ameiambia BBC kwamba ufisadi huo ulisababisha vifo vya maelfu ya raia wa Nigeria.
Wanajeshi wa taifa hilo wamelalamika kwamba licha ya kiasi kikubwa cha fedha kinachotumiwa kununua vifaa vya kijeshi hawana vifaa vya kuweza kukabiliana na kundi la Boko haram.

Toka Ufaransa...Polisi wavamia washukiwa wa mashambulio Paris...


Washukiwa wawili wamefariki baada ya maafisa wa usalama kushambulia Saint Denis kaskazini mwa Paris, wakisaka waliohusika mashambulio ya Ijumaa.
Ufyatulianaji mkali wa risasi umetokea mapema asubuhi kwenye mtaa huo. Operesheni hiyo inadaiwa kumlenga mwanamgambo wa Islamic State Abdelhamid Abaaoud ambaye amedaiwa kupanga mashambulio hayo yaliyoua watu 129.
Maafisa kadha wa polisi wamejeruhiwa kwenye operesheni hiyo, kituo cha runinga cha BFMTV cha Ufaransa kimeripoti.
Video iliyoonyeshwa na vituo vya televisheni vya BFMTV na iTele zimeonyesha watu walioshuhudia wakisema milio ya risasi ilianza kusikika saa kumi unusu alfajiri saa za Ufaransa.
Naibu meya Stephane Peu amewahimiza raia wasalie manyumbani, akisema "hili si shambulio jipya bali ni operesheni ya polisi".

Awali, duru za kiusalama zilisema video ya kiusalama ilikuwa imeonyesha huenda kulikuwa na mshambuliaji wa tisa mashambulio hayo ya Ijumaa.
Watu 129 walifariki kwenye mashambulio yaliyotokea maeneo sita mjini Paris.
Kundi la Islamic State (IS) limesema ndilo lililotekeleza mashambulio hayo.
Ripoti moja inasema barabara zimefungwa eneo la Place Jean Jaures mtaa wa Saint Denis.
Uwanja wa taifa wa michezo wa Stade de France, ambako washambuliaji walilipua mabomu Ijumaa, umo kwenye mtaa huo.

UJANGIRI NCHINI TANZANIA BADO UNAENDELEA... KOBE 201 WANASWA WAKISAFIRSHWA NJE YA NCHI UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA J.K NYERERE........


Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.
Adelhelm Meru akikagua mabegi matano yenye Kobe 201 yaliyokamatwa usiku wa
kuamkia leo na askari wanyamapori kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na
usalama katika uwanja wa Kimataifa wa J.K. Nyerere jijini Dar es Salaam.  
 
Watuhumiwa
hao wa usafirishaji wa wanyamapori wametajwa kuwa ni David Mungi mkazi wa
Muheza Mkoani Tanga na Mohammed Suleiman (43) mkazi wa Zanzibar ambao katika
tukio hilo walishafanikiwa kupita kwenye mitambo ya ukaguzi lakini mbwa maalum
(sniffer dogs) wakasaidia kugundua uhalifu huo. Kwa pamoja watuhumiwa hao
walikamatwa na tiketi za kusafiria kuelekea nchini Malaysia. 
 
Kobe wapatao 201 waliokamatwa na askari wanyamapori kwa ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutumia mbwa maalum (sniffer dogs).   
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Dorina Makaya kulia na Mmoja wa Askari wanyamapori wakiangalia kobe 103 waliotelekezwa eneo la Tabata hivi karibuni
baada wahalifu waliohusika kuhofia kukamatwa na vyombo vya dola. 

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM SAIDI MECK SADIKI MGENI RASMI SIKU YA WATOTO NJITI JIJINI DAR ES SALAAM..2015..........

Mkuu wa  Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki (wa pili kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa (wa nne kulia)   mashine ya kutoa hewa ya Oxygen kwa watoto waliozaliwa kabla ya wakati Oxygen Concentrator) kwaniaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru, kuanzia kulia ni mwakilishi Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Grace Mallya, Kaimu Mkuu wa Idara ya Watoto na Dk, Bingwa wa Watoto, Martha Mkony na anayefuatia ni Doris Mollel ambaye ni 
Mwakilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation
Baadhi ya wafanyakazi
Baadhi ya wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili
 
 
Afisa Mrakibu Mwandamizi wa Magereza (SSP) akizungumza jambo wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Watoto njiti Dar es Salaam
Mkazi wa Mbagala  Kizuiani Jijini Dar es Salaam, Jesca Yusuph akiwashukuru madaktari na wauguzi pamoja na Mwanzilishi wa Taasisi ya (DMF)
 
Mkuu wa Mkoa Saidi Meck Sadik na Mtoto Amney Salimu (3) akiwa amebebwa na mama yake mzazi Eshe Ahmed, wakikata Keki  wakati wa siku ya Watoto Njiti,  Dar es Salaam, wa pili kulia ni Mwakilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation na wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Uuguzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,  Agnes Mtawa
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Saidi Meck Sadik akilishwa Keki na  Mtoto Amney Salimu (3) akiwa amebebwa na mama yake mzazi Eshe Ahmed, wakati wa siku ya Watoto
Njiti Dar es Salaam, wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Taasisi ya Doris
Mollel Foundation na watatu  kushoto ni Mkurugenzi wa Uuguzi katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,  Agnes Mtawa

RASMI JANA MH:JOAB NDUGAI USPIKA WA BUNGE LA TZ 2015....

nd1
Spika wa Bunge la Kumi na Moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai akiongoza kikao cha kwanza cha Bunge hilo jana mara baada ya kuchaguliwa na wabunge.
nd2
Mgombea wa Uspika wa Bunge la Jamhuri kutoka Chama cha Wakulima Tanzania Peter Leonard Sarungi akiomba kura kwa wabunge.
nd3
Mgombea wa Uspika kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Goodluck le Medeye akiomba kura kwa wabunge
nd4
Watumishi wa Bunge wakionesha masanduku matupu ya kura za Spika
nd5
Baadhi ya watumishi wa Bunge wakigawa karatasi za kupigia kura ya Spika kwa wabunge.
nd7
Baadhi ya wabunge wakipiga kura ya Spika
nd10
Spika Mteule wa Bunge Job Ndugai akiongozwa na askari wa Bunge baada ya kutangazwa Mshindi na Mwenyekiti wa Bunge wa Muda Andrew Chenge baada ya kupata kura 254.
nd11
Mbunge Andrew Chenge akila kiapo cha Uaminifu cha Ubunge
nd12
Mbunge Richard Ndassa akila kiapo
nd13
Mbunge Mary Nagu akila kiapo
nd14
Mbunge wa Kuteuliwa Dkt. Tulia Ackson akila kiapo
nd15
Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Upendo Peneza akila kiapo
Picha zote na Hussein Makame

Je Ni Sawa kusikiliza muziki wa R Kelly baada ya kujua alikuwa na mahusiano na binti mwenye miaka chini ya 18 ?.....



r kelly
Kuelekea kutoka kwa album yake ya 13 ‘The Buffet’ rnb staa R Kelly amefanyiwa mahojiano hivi karibuni na jarida la New York  kuhusu tabia na skendo yake ya zamani ya kuwa na mahusiano na mabinti wenye umri chini ya miaka 18.
Swali kubwa lilikuwa Je Ni Sawa kusikiliza muziki wa R Kelly baada ya kujua au kudhani anatabia hii ?
Kila siku ni takuwa ni zawadi kwa watu ila hilo litabaki kuwa laana kwangu, watu milioni moja wananiongelea vibaya ila milioni nane wananipenda,so nina watu milioni tisa wanaoniongelea,hio inanifanya nizidi kubaki kwenye muziki “.
Mwandishi wa habari za burudani mjini Chicago alifanyiwa mahojiano na jarida hili pia na kusema ” Sio sahihi kuhusisha maisha binafsi ya msanii na Muziki au sanaa yake, kama unapenda sanaa yake baki kuwa shabiki “.
R Kelly pia ameulizwa kama bado anatamani kuwa na mabinti wenye umri chini ya miaka 18 ?
Kelly alijibu kwa kusema ” huo ni uzushi kama uvumi mwingine tu duniani, ndio maana siongelea mambo hayo, ningekuwa mtu wa kawaida haya mambo yasingeongelewa kuhusu mimi  “.

Matokeo ya Mtanange kati ya Algeria Vs Taifa Stars November 17 2015........


Ronaldo anamuiba binti wa wakala wake …….

Cristiano Ronaldo kuingia katika headlines imekuwa kawaida sana kwake ukilinganisha na Lionel Messi ambaye amekuwa akitajwa kama mshindani wake mkubwa licha ya kuwa maisha binafsi wako tofauti sana kitabia za nje ya uwanja. Ronaldo amekuwa akihusishwa sana kuwa katika mahusiano na wapenzi wengi kwa nyakati tofauti tofauti.
2E89F8EC00000578-3322398-image-a-44_1447782766649
Ronaldo katika picha ya pamoja akiwa na wakala wake Jorges Mendes pamoja na Marisa Mendes wakati wa uzinduzi wa movie ya Ronaldo
Amewahi kuripotiwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi ya muda mfupi na Kim Kardashian lakini Paris Hilton amewahi kutoka na staa huyo, mrembo kutoka katika mchezo wa tennis Maria Sharapova na baadae Iryna Shayk ila headlines za November 17 zinazo muhusu staa huyo anatajwa kutoka kimapenzi na Marisa Mendes ambaye ni binti wa wakala wake Jorges Mendes.

Magazeti 15 ya Tanzania November 18 2015

Thursday, November 12

Ndoa za Utotoni Zaendelea Kushamiri Nchini-Katav

RPC1
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari

Hii stori imegusa kwenye vichwa vya habari za Magazeti ya Tanzania November 11 2015, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, na kasimulia stori ilivyokuwa mwanzo mwisho mpaka wakapata taarifa kuhusu mpango wa ndoa kufungwa kati ya msichana mwenye umri wa miaka 14 na mvulana mwenye umri wa miaka 17. 

Tulipata taarifa kutoka Kijijini kwao kutoka kwa wananchi ambao hawakufurahia hicho kitendo, tukaweka mtego wa kufuatilia.. tulifanikiwa kupata watuhumiwa ambao ni kijana anayeoa, baba na mama mzazi wa muoaji, na mwalimu ambaye alihusika na alijua mkakati unaoendelea kwa mwanafunzi wake“-Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, RPC Dhahiri Kidavashari.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi akaendelea na sentensi nyingine >>> “Wamekamatwa na sasahivi wako kituoni, taratibu za kuwafikisha Mahakamani zinaendelea“- Dhahiri Kidavashari.

Kisheria hii ishu ya ndoa ikoje? Majibu ya RPC haya hapa >>> “Kisheria ilitakiwa iridhiwe na wazazi, kuna Sheria tatu, Sheria ya ndoa, Sheria ya dini na Sheria za kimila… kisheria mtu yoyote chini ya miaka 18 hana ridhaa ya kuamua ndoa, halafu huyo ni mwanafunzi aliyesajiliwa kufanya mtihani.. Tuheshimu haki za Kikatiba za kila mtu, kusoma ni haki ya kila mtu na wazazi wana wajibu wa kusomesha watoto… ni ng’ombe 11 tu zilizotelewa ili aolewe“- Dhahiri Kidavashari.

Friday, October 23

TAARIFA YA MKUU WA MKOA WA DODOMA CAPT CHIKU GALLAWA KUHUSU UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 25, 2015 MKOANI DODOMA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
Mkoa wa Dodoma
Anwani ya Simu REGCOM
Simu Nambari: 2324343/2324384
E-Mail No. ras@dodoma.go.tz
Fax No. +255 026 2320046
          
  Kateni Msitaafu Chiku Gallawa [RC]
    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,
                            S.L.P.  914,
                              DODOMA.
Ndugu wananchi wa Mkoa wa Dodoma, tarehe 25 Oktoba, 2015 ni siku ya Uchaguzi Mkuu hapa nchini; ambapo, Watanzania wale wenye sifa za kupiga kura na waliojiandikisha, watapata fursa na kutumia haki yao ya kikatiba kuchagua viongozi mbalimbali wa nchi yetu, kuanzia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani.
Maandalizi ya kufanikisha zoezi la Uchaguzi Mkuu kwa Mkoa wa Dodoma yamekamilika. Hadi kufikia siku ya leo tayari wasimamizi wa uchaguzi wa wilaya zote saba za Mkoa wa Dodoma wameshapokea vifaa vyote vitakavyo tumika kwenye zoezi la uchaguzi. 
 
Hadi tunavyozungumza sasa, vifaa hivyo vinapelekwa kwenye vituo vya kupigia kura.
Vilevile, wasimamizi wa uchaguzi kwenye wilaya zote saba za Mkoa wa Dodoma wameshapokea fedha za kuendeshea uchaguzi Mkuu.  Aidha, Mafunzo kwa watendaji wote watakaoshiriki katika zoezi la uchaguzi yanahitimishwa kwenye wilaya za Dodoma.
 
Mkoa wa Dodoma tumefanikiwa kuandikisha jumla ya wananchi 1,053,136 kuwa wapiga kura sawa na asilimia 102.74 ya lengo, ambapo lengo ilikuwa kuandikisha watu/wapiga kura 1,025,084, Hivyo, natumia fursa hii kuwataka wale wote waliojiandikisha kupiga kura katika Mkoa wa Dodoma, kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya Jumapili Oktoba 25. 
 
Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa kuanzia saa 1:00 asubuhi na zoezi la kuhesabu kura litaanza saa 10:00 jioni.  
Natumia fursa hii kusisitiza mambo machache ya muhimu kwenye zoezi la uchaguzi Mkuu mwaka 2015 kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma na wadau mbalimbali wanaoshiriki Uchaguzi Mkuu kama ifuatavyo:
·        Wananchi wale wenye sifa za kupiga kura, wanahimizwa kwenda kupiga kura kwa amani na utulivu kwa kuzingatia muda na kisha kurejea makwao/majumbani baada ya kumaliza kupiga kura.
 
·        Viongozi wa vyama vya siasa na wagombea wa nafasi mbalimbali wawaandae wanachama na wafuasi wao kwenda kupiga kura, bila kuvunja sheria za uchaguzi, taratibu na kanuni zilizowekwa; wakidumisha hali ya Amani na utulivu.
 
·        Hairuhusiwi kwa mtu yeyote siku ya uchaguzi kufanya kampeni ya aina yoyote wala kuvaa mavazi ya chama chochote cha siasa.
 
·        Hairuhusiwi kwa mtu yoyote kutoa Rushwa kwa lengo la kumshawishi mtu kupiga kura au kumshawishi asipige kura.
 
·        Kila mtu aliyejiandikisha kupiga kura atunze shahada yake ya kupigia kura na asiitoe kwa mtu mwingine wala yeye kutumia shahada ya mtu mwingine kwani ni kosa la jinai kutumia shahada ya mtu mwingine kupigia kura. vilevile ni kosa kutumia shahada bandia.
 
·        Ni vizuri kila mmoja akahakikishe jina lake kwenye kituo alichojiandikishia ili kupata uhakika wa kuwepo kwenye orodha na kupiga kura kabla ya siku ya kupiga kura Oktoba 25.
 
·        Wananchi wote wakae katika hali ya utulivu wasiwe na hofu wala woga, Jeshi la polisi litafanya doria mbalimbali zenye lengo la kuhakikisha kunakuwa na hali ya Utulivu na hali ya Amani ili kila mtu apate fursa ya kushiriki zoezi la Uchaguzi.
Kabla sijahitimisha salamu zangu, narudia kuwasisitiza Wananchi wote wa Dodoma wale wenye sifa za kupiga kura wajitokeze kwa wingi kupiga kura siku ya Jumapili, Serikali imejiandaa vya kutosha na kuwahakikishia wananchi uchaguzi Mkuu kufanyika kwa amani, utulivu na kuwa uchaguzi wa Huru na Haki.
 
Nawaomba wananchi wote wajiepushe na vitendo vyovyote vinavyosababisha vurugu na Uvunjifu wa Amani; tuendeleze sifa yetu ya Mkoa wa Dodoma kufanya Uchaguzi tukiwa katika hali ya usalama.
Mwisho kabisa, nawatahadharisha wale wote wenye nia mbaya au wanaojipanga kutaka kujaribu kuvuruga zoezi la uchaguzi au kuleta vurugu ya aina yoyote hapa Mkoani Dodoma kuwa,  vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga imara na vitamshughulikia mara moja mtu huyo. Wananchi mnaombwa kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama au kwa kiongozi yoyote wa eneo husika.
Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.
Imetolewa na:
OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA
Oktoba 23, 2015

BAADA YA MADAI YA UTOVU WA NIDHAMU HII NDIO KAULI YA DIEGO COSTA

Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Diego Costa ambaye amekuwa akiingia katika headlines kutokana na baadhi ya matukio yake anayoyafanya uwanjani, October 23 ameingia katika headlines tena baada ya kusema kuwa hawezi kubadilika kutokana na watu wanavyotaka na kufikiria.

Diego Costa amekuwa akiingia katika headlines kutokana na vitendo vyake vya utovu wa nidhamu, Diego Costa tayari alishafungiwa mechi tatu mwaka huu katika vipindi viwili tofauti tofauti. Costa alifungiwa mechi tatu kutokana na kugombana na beki wa Arsenal Laurent Koscielny na kumkanyaga kwa makusudi beki wa Liverpool Emre Can.

“Sitobadilika hivyo kwa sababu ya watu wanavyoweza kufikiria, baadhi ya watu wanaweza kufikiria mchezo wa mpira wa miguu ni kama ukumbi wa michezo kuwa kila mmoja anaweza kufanya vizuri. Lakini nafikiria mtu hubadilika pale unapovuka mstari mweupe wa kuingia uwanjani na unakuwa mtu tofauti na pale unapokuwa nje ya uwanja, ila ninapokuwa uwanjani naenda kupambana kwa ajili ya timu yangu na kuhakisha nafanya vizuri”>>> Diego Costa

MAHAKAMA: MARUFUKU MITA MIAMBILI, PIGA KURA, RUDI NYUMBANI

Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam imetoa maamuzi ya kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na kada wa Chadema aliyekuwa akiiomba mahakama hiyo kutoa uamuzi wa kwamba wananchi wanatakiwa kukaa mita ngapi baada ya kupiga kura.


Mahakama hiyo imelitolea suala hilo ufafanuzi na kusema kuwa ni marufuku kwa wananchi kukusanyika katika kituo cha kupigia kura na hata njee ya mita 200 hairuhusiwi kwani ni kinyume cha sheria.


Kesi hiyo namba 37 ya mwaka huu, ilifunguliwa na mgombea ubunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chadema, Amy Kibatala, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) chini ya hati ya kiapo cha dharura.


Oktoba 16, mwaka huu, mlalamikaji alifungua kesi ya kikatiba iliyopewa usajili namba 37, ya mwaka huu akiiomba Mahakama itoe tafsiri ya kifungu cha 104 kidogo cha (1) cha Sheria ya Uchaguzi kama kinazuia ama kuwaruhusu wananchi kukaa kwa utulivu umbali wa mita 200, baada ya kupiga kura katika vituo.

Monday, October 19

AU YAUNDA JESHI LA PAMOJA AFRIKA



Kikosi kipya cha majeshi ya umoja wa Afrika kinafanya mazoeozi yake ya kwanza hii leo nchini Afrika Kusini.

Mazoezi hayo yanalenga kutathmini utayari wa kikosi hicho kutumika wakati kunapotokea dharura na kunahitajika kikosi cha mbele kitakachodhibiti hali na kuokoa maisha ya watu.

Lakini swali ibuka ni je jeshi hilo litatumwa katika taifa lililochangia wanajeshi wake ?

Mwandishi wa BBC anayeshughulikia maswala ya kiusalama Tomi Oladipo, anasema kuwa madhumuni ya kikosi hicho cha wanajeshi 25,000 kutoka mataifa ya bara Afrika ni kupunguza kutegemea kwa majeshi ya mataifa ya ulaya kuja humu barani kusuluhisha migogoro inayotokea.




Kikosi hicho kinatarajiwa kuanza oparesheni yake ya kwanza mwezi januari mwakani.

Hata hivyo umoja wa Afrika unasema unahitajika takriban dola bilioni moja kufadhili shughuli na oparesheni za kikosi hicho.

Mwandishi wa BBC anayeshughulikia maswala ya kiusalama anasema kuwa kuna changamoto za ukosefu wa ushirikiano mwema baina ya mataifa shirika.




Vilevile anasema kuwa mataifa mengi hayajajitolea kuunga mkono jeshi hilo kisiasa.
Jeshi hilo linatarajiwa kuwa na vikosi vitano.

Kwa sasa Cameroon imejitolea kuwa mwenyeji wa kikosi hicho ikisema watakita kambi yao katika mji wa Douala.

                                             bbcswahili.com